Na Yego Sholla Golikipa wa Liverpool Loris Karius amesema kwamba kushindana na Simon Mignolet " Sio Rahisi " na ameweka wazi kwamba hana majuto yoyote ya kuondoka Manchester City akiwa mdogo. Golikipa huyo wa Kijerumani alitua Anfield Agosti ya 2016 na baada ya maandalizi ya msimu ya majira hayo ya kiangazi ambayo yalimuweka nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu , sasa hivi amechukua namba moja ndani ya kikosi cha Jurgen Klopp. Hata hivyo baada ya kuonyesha kiwango cha chini kwa baadhi ya mechi , karius amejikuta akishindana na Simon Mignolet kuwania nafasi ya kuanza golini , lakini akiwa anafurahia kucheza mechi nyingi golini mpaka sasa bado anakabiliwa na wakati mgumu wa kushindana na mwenzake. " Nilipofika, haikuwa rahisi. Nilijua baada ya msimu wa kwanza ambao nilianza na majeraha , na nikarudi golini tena na kucheza baadhi ya mechi , halafu nikatoka tena kikosini , Simon akarejea na akafanya vizuri na timu ikafuzu kucheza UEFA , nilijua kwamba kutakuwa na uw...