MIGNOLET SIO RAIS KUSHINDANA NAYE :LORIS KARIUS
Na Yego Sholla
Golikipa wa Liverpool Loris Karius amesema kwamba kushindana na Simon Mignolet " Sio Rahisi " na ameweka wazi kwamba hana majuto yoyote ya kuondoka Manchester City akiwa mdogo.
Golikipa huyo wa Kijerumani alitua Anfield Agosti ya 2016 na baada ya maandalizi ya msimu ya majira hayo ya kiangazi ambayo yalimuweka nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu , sasa hivi amechukua namba moja ndani ya kikosi cha Jurgen Klopp.
Hata hivyo baada ya kuonyesha kiwango cha chini kwa baadhi ya mechi , karius amejikuta akishindana na Simon Mignolet kuwania nafasi ya kuanza golini , lakini akiwa anafurahia kucheza mechi nyingi golini mpaka sasa bado anakabiliwa na wakati mgumu wa kushindana na mwenzake.
" Nilipofika, haikuwa rahisi. Nilijua baada ya msimu wa kwanza ambao nilianza na majeraha , na nikarudi golini tena na kucheza baadhi ya mechi , halafu nikatoka tena kikosini , Simon akarejea na akafanya vizuri na timu ikafuzu kucheza UEFA , nilijua kwamba kutakuwa na uwezekano mwanzoni mwa msimu huu angeanza tena golini ."
" Sio rahisi kwa Golikipa kutoka na kurejea Golini kila mara , lakini hiyo ndio ilikuwa hali halisi , lazima uikubali na kuifanyia kazi."
" Maisha ya Golikipa huwa unakosolewa sana pale unapokuwa na siku mbaya kwahiyo inabidi uzoee tu na katika klabu kama hii ni zaidi ya vile nilivyozoea kule nilipotoka kwahiyo labda hilo ndio lilikuwa jambo kubwa sana."
Sio kwa mara ya kwanza kwa Karius kucheza Uingereza , alitumikia Man City kwa miaka miwili katika umri wa miaka 16 lakini hakuwahi kucheza kikosi cha kwanza , na kupelekea kuondoka na kutafuta mahala pa kucheza.
" Nilicheza katika kikosi cha chini ya miaka 18 na kikosi cha wachezaji wa akiba na kuna muda nilikuwa nafanya mazoezi na kikosi cha kwanza na Joe Hart ambaye alikuwa mtu mzuri sana alinisaidia sana. Na sijutii chochote."

Comments
Post a Comment