Posts

Showing posts with the label Movie

PICHA 8: MUONEKANO MPYA KWA SASA WA JENNIFER NA PATRICK WALIOIBULIWA NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Image
Watu wengi watawakumbuka Jennifer na Patrick kwa jinsi walivyoweza kutikisa tansia ya filamu Tanzania kipindi cha nyuma walipoibuliwa na marehemu Steven Kanumba. Watoto hawa wawili walicheza kwa ustadi mkubwa katika filamu za Uncle JJ na This is It zote za marehemu Kanumba. Kwa sasa Hanifa Daud ‘Jennifer’ na Othman Njaidi ‘Patrick’ si watoto tena. Wawili hawa hawajaonekana sana kwenye filamu baada ya Steven Kanumba aliyewatoa kufariki. Jennifer ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana mara ya mwisho alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu a.k.a Nisha mwaka 2014. Kwa upande wake Patrick, yeye alisema kuwa hana shauku ya kuigiza tena kama ilivyokuwa awali. Credit: Bongo5

ITAZAME HAPA BURE FILAMU YA JENNIFER MGENDI & BAHATI BUKUKU -TEKE LA MAMA SHARE NA WENGINE

Image

Aunty Ezekiel aiachia sokoni filamu mpya ‘Christmas Eve’

Image
Mara nyingi kwenye msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya, waigizaji duniani huingiza sokoni filamu zinazoendana na wakati huo. Ni nadra sana kwa waigizaji wa Tanzania kuja na filamu za aina hiyo. Lakini si kwa Aunty Ezekiel, ambaye mwaka huu ameachia filamu iitwayo, Christmas Eve. Muigizaji huyo na mama wa mtoto mmoja aliyezaa na dancer wa Diamond, Mose Iyobo, ameshirikiana waigizaji wengine wakiwemo Husna Iddy, Lissa Tarimo, Vivian Minja na wengine kucheza filamu hiyo. “Usiamini kila kitu unachokiona au kusikia….. Kwasababu kila hadithi Ina pande Tatu yao, yako, Na ukweli,….. Christmas eve bonge LA movie iko mtaanii now …. Go get ur og copy,” ameandika muigizaji huyo kwenye Instagram.