Posts

Showing posts with the label Habari Mpya

INIESTA KUWAKOSA CHELSEA

Image
    Na Yego Sholla Taarifa kutoka SkySports zinasema Barcelona wamethibitisha kumkosa kiungo mshambuliaji INIESTA ni baada ya amepata jeraha katika mguu wake wa kulia katika kipindi cha kwanza baina ya Atletico Madrid na Barcelona waliibuka washindi wa 1-0 dhidi ya Atletico Madrid. Klabu ya barcelona itawaalika Chelsea katika dimba la la Barcelona march 14 mwezi huu mpambano wa kwanza pale nchini Uingereza ulimalizika kwa kutoshana nguvu ya 1-1 Kocha wa klabu hiyo ya Barcelona Ernesto Valverde ameiambia Tovuti ya klabu : " Bila Iniesta, tunapoteza mchezaji wa kipekee, pengo lake halizibiki." " Ni ngumu kutafuta mbadala wake, kwasababu hakuna kama yeye Duniani. Ngoja tuwe na tumaini kwamba jeraha lake sio kubwa."

SOKO LA KAYANGA KARAGWE LATEKETEA KWA MOTO

Image
Soko la Kayanga Karagwe lateketea kwa moto chanzo moto huo kikiwa hakijajulkana endelea kuwa nasi kupata taarifa kamili pale wapelelezi watakapomaliza kazi yao

MVUA KUBWA YA MAWE ILIYOAMBATANA NA UPEPO MKALI YASABISHA MADHARA MAKUBWA WILAYANI KYERWA KIJIJI KAGENYI

Image

News:kutoka Mjini Bukoba.

Image
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika manispa ya bukoba maarufu kwa jina la wamachinga waliokuwa wameondolewa kwenye maeneo ya kingo za barabara zilizoko katika maanispaa hiyo baada ya kutengewa eneo la machinjio ya zamani kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kibiashara leo wameyavamia tena maeneo ya kingo hizo za barabara na kupanga bidhaa zao kwa kisingizio cha kwamba Rais Magufuli ameagiza wasibugudhiwe. Wamachinga hao huku wakiimba nyimbo za kumsifu Rais John Pombe Magufuli wamesema wamelazimika kuyavamia maeneo ya kingo za barabara baada ya kusikia agizo la rais la kutaka wasibugudhiwe kwa kuwa eneo la machinjio ya zamani lilitengwa na manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kuendesha biashara ya kuwa lilikuwa sio rafiki kwao. Mapema 6 Desemba 2016 Rais Dkt. John Magufuli alimuagiza Waziri na Katibu Mkuu Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja mpango wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo (MACHINGA) jijini Mwanza na mikoa mingine nchini, h...

Mchezaji mwingine aanguka na kuzimia uwanjani, akimbizwa hospitali

Image
Siku chache baada ya kinda wa Mbao FC timu ya vijana U 20 kuanguka uwanjani na kupoteza maisha, mchezaji mwingine ameanguka na kuzimia. Katika hali isiyotarajiwa, beki wa timu ya Colombia FC ya Mwananyamala, Athumani Suwa, jana asubuhi alikata kauli baada ya kuzimia uwanjani kutokana na kugongana na mwenzake wakati wakiwania mpira kabla ya kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar. Tukio hilo lilitokea katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B, Dar.Baada ya kufika hospitalini hapo na kushuhudia mchezaji huyo akiwa amewekwa katika chumba cha mapumziko baada ya kupatiwa huduma. Akizungumza mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye alikuwepo katika mazoezi hayo, Ramadhan Ally, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo uwanjani.

Moto Mkubwa wawaka Mkoani Kagera Bukoba Mjini

Image
Mjini Bukoba Maduka mawili yaliyopo katikati ya MAKUTANO ya mtaa na Zamzam na Arusha Jirani na Soko kuu yashika moto na mengine yaliyopo jirani kuathirika na moto huo ingawa juhudi za wenye maduka za kuokoa mali zimefanikiwa kuepusha hasara zaidi Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Oct 28 majira ya saa 2:00 na kupelekea Askari wa Kikosi cha Zimamoto,kunusurika kichapo kutoka kwa baadhi ya wananchi baada ya kuchelewa kufika eneo la tukio.  Bwana Emiry Baruti mmiliki wa Jengo lililopata moto.  Wananchi wakikimbizana na ndoo za maji kusaidia kuuzima moto huo Gari la zima moto likiwa limefika eneo la tukio baada ya muda  Mpaka tunaingia mitamboni Chanzo cha moto huo hakijajulikana  Kijana Evody akijaribu kuokoa mali kutoka katika Duka lake lililopo katika Jengo lililoshika moto Mali zikiendelea kuteketea kwa moto  Mali zilizo okolewa katika Duka la Kijana Evody Dogo Ditto  Moto ukiendelea kuchukua kasi katika chumba c...