Posts

Showing posts with the label Miaka 55 ya Uhuru

HII HAPA DROO YA RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA

Image
BOFYA HAPA KUDONWLOAD NIJUZEHABARI BLOG Youvil Town ambayo ni timu ya nafasi ya chini zaidi iliyosalia katika michuano hii itawakaribisha Manchester United. Tottenham watakutana na Newport County. Vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City itakuwa ugenini kucheza na Cardiff City au Mansfield Town, huku Nottingham Forest iliyowatoa mabingwa watetezi Arsenal itakutana na Hull City. Raundi ya nne ya Kombe la FA itachezwa wiki ya Januari 26-29. Timu nyingine ni kama unavyoona hapa chini: Liverpool v West Brom Peterborough v Fleetwood/Leicester Huddersfield v Birmingham Notts County v Wolves/Swansea Yeovil v Manchester United Carlisle/Sheffield Wednesday v Stevenage/Reading Cardiff/Mansfield v Manchester City MK Dons v Coventry Millwall v Rochdale Southampton v Watford Middlesbrough v Brighton/Crystal Palace Bournemouth/Wigan v Shrewsbury/West Ham Hull v Nottingham Forest Newport County v Tottenham Norwich/Chelsea v Newcastle Sheffield United v...

Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Image
Wakati Tanzania Bara ikielekea kuadhimisha miaka 55 ya uhuru wake hapo kesho, jamii ya Watanzania imetakiwa kujitathmini na kubadilika hasa katika kutunza mali za serikali. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na EATV pamoja na East Africa Radio kuhusu maandalizi ya sherehe hizo. Mhe. Jenista amesema vitendea kazi na miundombinu iliyojengwa kwa kodi za wananchi ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kuvithamini ili vilete mabadiliko katika kufikia malengo ya nchi. Akizungumzia maandalizi ya sherehe za kutimiza miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania amesema tayari kila kitu kimekamilika sambamba na mialiko kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa imeshawasilishwa kwa viongozi hao. Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 9 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar...