Posts

Showing posts with the label Makala

WAAMUZI WA KIINGEREZA KUTOWEPO URUSI.

Image
Na Yego Sholla Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 80, nchi ya Uingereza haitakuwa na mwamuzi kwenye michuano ya kombe la dunia. Lakini ni UK nzima kwa maana ya Uwelshi, Uskochi, na Jamhuri ya Ireland. Lakini gumzo kubwa lipo Uingereza maana hata kiuwezo lenyewe ni taifa kubwa kimpira ukilinganisha na hayo mengine. Wana ligi inayofuatiliwa zaidi na wamekuwa na kawaida ya kuamini kuwa ubora wote uko kwao pia. Promo na vitu kama hivyo na ndio maana kuna mshtuko miongoni mwa wengi kuwa hawana hata mwamuzi mmoja kwenye michuano hii. Sababu ambayo wengi watakupa ni kwamba ubora wa waamuzi kutoka nchini humo umepungua. Hili linaweza kuwa kweli lakini hebu tuangalie vizuri na mengine. Kikawaida mwamuzi huwa anasemekana kufikia kilele cha uamuzi pale anapofanikiwa kuchezesha fainali ya michuano mikubwa zaidi ya soka Ulimwenguni. Na hili huwa liko wazi kutokana na ubora wa mwamuzi husika kwenye kuchezesha soka la ngazi mbali mbali hapo kabla. Hivyo basi waamuzi kutoka Uingereza ndio wam...

NEMBO YA BRAZIL INAVYOMDAI NEYMAR

Image
Na Yego Sholla Hakuna kitu kinachomuumiza kichwa Neymar na wafuasi wake kwa sasa kama hili jeraha la kifundo alilonalo linaloweza kumfanya ashindwe kucheza kwenye kombe la Dunia au hata ashindwe kuwa kwenye ule ubora wake hata akiweza kusimama kwenye kiti alichokalia sasa. Kwa miaka mingi Brazil wamekuwa na "Icons" kwa maana ya wachezaji ambao ndio nyota zaidi nchini humo kwa wakati fulani. Walipita kina Pele, Ronaldinho na kwa sasa ni yeye. Namba 10 za Brazili ndio zimekuwa Icons kwenye vizazi tofauti tofauti lakini wote walipata heshima kubwa ikiwemo kushinda Kombe la Dunia na Ballon D'or.  Heshima za kuwa Nembo walikuwa nazo. Kwa sasa Neymar ndio amebeba mzigo huo. Kwa kuanzia alihitaji kujitoa kwenye kivuli cha Lionel Messi pale Barcelona maana ni wazi huwezi kuwa mchezaji bora wa Dunia kama wewe hata sio nyota kwenye timu unayocheza. Nadhani hilo liko wazi. Hatua ya kwenda PSG imempa uhuru wa kutawala lakini kuwa pale kunamlazimu afanye mambo makubwa na ya ki...

UNAFIKI, UROHO WA MADARAKA UNAIPELEKA TFF SHIMONI

Image
Na Joseph michael Thursday, March 29, 2018 TAKRIBANI wiki mbili sasa ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hakuna jambo la maendeleo ambalo linazungumziwa badala yake mizengwe na kuchafuana. Gumzo la nani hafai na nani anafaa ndiyo limechukua sura kubwa ya maisha mapya ya TFF ambayo ninaamini wako waliokuwa na matumaini makubwa kuhusiana na suala la maendeleo. Kuna mambo mengi sana hayana majibu na huenda yametumika kuwabadilisha wengi walioamini chini ya Urais wa Wallace Karia, basi mambo yatakwenda vizuri kabisa. Kwa sasa gumzo ni aliyekuwa Makamu Rais wa TFF, Michael Wambura ambaye amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka akipatikana na tuhuma kadhaa ikiwa ni pamoja na kupokea malipo ambayo yanaonekana hayakuwa sahihi, pia kushusha hadhi ya shirikisho. Wambura amekuwa akipinga hilo na ametumia nguvu kubwa huku akieleza mambo mengi yakiwemo mengine ambayo yanaonekana si ya msingi kwa kuwa anayesema baada ya kuona ameondolewa wakati akiwa ndani ya TFF hakuw...

BAYERN MUNICH NA SILAHA ROBERT LEWANDOWSKI KATIKA NJIA ZA ALEXANDER THE GREAT.

Image
I Na Yego Sholla Kati ya mwaka 336–323 kabla ya kuzaliwa Kristo, utawala na nchi ya Macedonia ulikua mkubwa sana. Chini ya Uongozi wa Kijana mmoja mtoto wa Mfalme Filippo II wa Macedonia na malkia Olympias Macedonia, Alexander The Great. Huyu alikua kiongozi, mtawala, mfalme na amri jeshi mkuu wa tawala yote ya Macedonia, Nchi iliyokua kaskazini wa Ugiriki ya kale. Alexander The Great anatajwa kama amri jeshi mkuu mashuhuri zaidi kuliko wote kwenye historia ya dunia. Huyu alianza kutawala himaya ya Macedonia mwaka 336 KK wakati huo akiwa na umri wa miaka 20 Tu mara baada ya baba yake Mfalme Filippo II kufariki kwa kuuwawa na mmoja kati ya walinzi wake. Mara baada ya kukalia kiti cha ufalme kazi ya Alexander The Great ilikua ni kuendeleza kile alichokianza baba yake kwa kuongeza zaidi himaya ya utawala wake. Akiwa kama kiongozi na amri jeshi mkuu, Alexander The Great alipambana vita nyingi ili kuhakikisha anashinda na kutawala sehemu kubwa ya dunia kuanzia Ulaya hadi Bara Hind...

MICHEZO YA KIMATAIFA KWA TANZANIA NA WAZO HURU KWA WADAU WA SOKA

Image
Na Yego Sholla Shirikisho aliwezi kuweka mkakati ambatanishi kwa michezo ya kirafiki kwa timu zake zote tano za mpira wa miguu kwa taifa moja ambalo litakuwa na mchezo huo. Mfano, Kama Congo anakuja kucheza mchezo wa kirafiki Basi aje na full package ya senior National team(wanaume na wanawake), Under 20(wavulana na wasichana), Under 17 na Under 15........ Mfano, Jana U17, U20, U15 zetu zingecheza kwanza na U15, U20, U17 za Algeria kabla ya Senior team kukutana. Nadhani tungepata experience na exposure kubwa Sana lakini pia hii ingetupa mwanya mzuri wa kufanya study tour kwa uendeshaji rafiki wa maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana. Hili Ni wazo tu..... Fedha zitumike Sasa hivi baadae zije zijirudishe..... Ukitizama kwa makini utagundua mpira wetu unakuwa zaidi kwenye program za vijana, huko ndipo ilipowekwa tija yetu kubwa na ninaopa tumaini kwa miaka ya baadae Kama elimu ya sayansi ya michezo itaelekezwa kwa hao vijana pia.

NAIONA TASWIRA YA TOWNSHIP ROLLERS KWENYE KIVULI CHA WOLAYTA DICHA

Image
Na Yego Sholla Kupangwa na timu kutoka ushelisheli ilikuwa furaha kubwa kwa Yanga kwa sababu furaha yao waliitengeneza kutokana na historia yao ya nyuma. Historia ya Yanga ilikuwa imeshiba dhidi ya hivi vilabu vya visiwani kama Comoro, Ushelisheli Haikuwa jambo la kushangaza kusikia Yanga wameitoa timu kutoka katika visiwa hivi kwa jumla ya magoli mengi. Kwao wao walikuwa wanajipigia wapendavyo, hakuna ambaye angeweza kuwazuia au hata kuwashauri kupunguza uzito wa vipigo kwa hizi timu. Jambo hili liliwafanya wapate viburi kwa kiasi kikubwa kila walipoona wanakutana na timu kutoka hizi sehemu. Hata walipokutana na St. Louis walijua kabisa jana inaweza ikawa na taswira ya leo, kitu ambacho kilikuwa tofauti sana. Ushindani waliokutana nao haukuwa ushindani ambao umezoeleka kwa kipindi cha nyuma, hakukuwepo na urahisi tena kwa Yanga kwenye mechi hii. Hadithi ya Yanga kuzitoa timu za ukanda huo kwa jumla ya magoli 2-1 ilikuwa hadithi ambayo ilikuwa haijazoeleka ka...

WACHEZAJI WANAOIHAMA ARSENAL WANA NUKSI

Image
Na Yego Sholla Aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Alexander Hleb aliwahi kusema mchezaji anaayehama Arsenal hawezi kufanikiwa anapoelelekea. Nadhani ndiye mtu aliwafumbua watu akili tukaanza kufuatilia kwa umakini wachezaji waliotoka timu hiyo kwenda timu nyingine. #ThieryHenry Huyu anachukuliwa all time best player wa EPL, alifanya kila kitu akiwa Arsenal na timu ya Taifa. Alichukua EPL,  FA, World Cup, akawa mchezaji bora EPL mara kadhaa na akakokosa uchezaji bora wa dunia. Wengi wanasema alikuwa na bahati mbaya kuzaliwa kipindi cha kina Zidane, Ronaldinho na De Lima. Alipoenda Barcelona pamoja na kuchukua La liga na CL hakuwa Henry wa Arsenal. Hakuchezeshwa kama mshambuliaji tena bali kama winger ya kushoto mbele akicheza Etto na baadae Zlatan. Hakuwa 'mungu' tena kama ilivyokuwa Highbury. Mwisho alienda kumalizia mpira wake Marekani. #VanPasie Huyu anachukuliwa kama mshambuliaji wa kuaminika baada ya Thiery Henry pale Arsenal. Aliondoka Arsenal kuelekea Man Utd msi...

WENGER NA HESHIMA YA KIFO CHA MKWAWA.

Image
Na Yego Sholla Chifu mkwawa wengi tumemsoma kwenye vitabu vya historia wakati tuko shule. Kwangu mimi huyu anabaki kuwa ni moja ya viongozi jasiri kabisa kuwahi kutokea hapa Afrika mashariki na hata kifo chake kimekuwa cha heshima kubwa sana. Kifo ambacho kinapaswa kuwa kama mfano wa hatma ya Arsene Wenger ndani ya Arsenal. Mkwawa alikuwa ni kiongozi wa kabila la Wahehe aliepingana na utawala wa Wajerumani enzi za ukoloni miaka ya 1800 mwishoni. Aliwapa shida sana ikiwemo kuua askari wengi sana na hata viongozi wao lakini hata pale alipoona amezingirwa hakusubiri akamatwe bali alijifyatulia risasi mwenyewe. Mkwawa hakusubiri auawe au kukamatwa na Wajerumani. Baada ya yote aliyowafanyia aliamini kuwa ni yeye tu ndio anastahili kuutoa uhai wake. Aliamini kukamatwa kwake ilikuwa ni ishara kuwa ameshindwa hivyo ni bora ajiue mwenyewe na sio wao kumkamata kwani aliona aibu sana. Mpaka leo fuvu lake lipo na anaheshima kubwa. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger wengi walipata kumwona ...

LIGI KUU YA UCHINA HATARI SANA YANASA KIFAA KINGINE TOKA LIGI KUU YA ENGLAND BOFYA HAPA KUJUA UNDANI WAKE

Image
Na Yego Sholla  Aliwahi kusema mwanahabari maarufu wa marekani Mignon McLaughlin kuwa sote tunazaliwa mashujaa, waaminifu na walafi lakini wengi wetu huwa tunabaki kuwa walafi. Ukisikia mchezaji yoyote ameenda kucheza China ujue huyo amefuata hicho cha mwisho akikwambia sijui timu alikuwa anaipenda na anaijua huyo ni mnafiki tu kwani wachezaji wangapi hata pale Ulaya huwa wanasema maneno hayo kila wakihamia timu mpya? Ndio maisha yalivyo bila unafiki hayaendi. Kivutio cha kwanza China ni pesa yao. Ubora wa ligi yao ni mdogo, hata wachina wenyewe hawajazi viwanja hivyo wakati wa mechi na hio ikutoshe kuwa hawavutiki na ligi yao. Pesa za wachina zinawapoteza na zinaelekea kupoteza ndoto za watu pia. Leo hii hakuna anaetaka kujua kuhusu Oscar wala Hulk. Au hata mchango wao kwenye timu zao. Ikusaidie nini? Ligi ya China inataka ikue kwa kuleta majina makubwa ya soka kutoka Ulaya lakini yenyewe ndio inayapoteza majina hayo kwa sababu ligi yao haina mvuto na mwisho nyota ...

JE WAJUA KWANINI MANCHESTER CITY NI BORA MSIMU HUU LIGI KUU YA ENGLAND BOFYA HAPA KUJUA UNDANI ZAIDI

Image
Na Yego Sholla Pengine unaweza kuja na jibu kuwa wapinzani wao ni dhaifu mno msimu huu. Lakini mimi naamini kuwa hili ni jibu sahihi pale v Bundesliga kwenye kesi ya Bayern Munich au hata PSG pale Ufaransa lakini sio pale Uingereza. Ubora wa Man city msimu huu hautokani na udhaifu wa wapinzani wao wakubwa bali matumizi sahihi ya pesa na mbinu za kiufundi. Pale Ujerumani pesa yote anayo Bayern ananunua mchezaji anaemtaka. PSG wana ubora mkubwa kitimu kuliko wapinzani wao lakini kwa Uingereza timu kubwa zina pesa na watu lakini zilishindwa kuwa na mikakati makini nazo. Ubora wa City haupo tu ndani ya uwanja bali nje pia na hapa ndipo wapinzani wote waliposhindwa lakini sio kwamba wao wamekuwa dhaifu sana, Hapana! Walikosa mipango na mikakati ya kuwa tofauti kama ilivyo kwa City. Ubora wa City ni matokeo chanya ya mikakati makini na ubora mkubwa wa rasilimali watu wake. Ubora wa Man city msimu huu unatokana na…. UWEKEZAJI Ni wazi kuwa fedha haichezi lakini inapowekezwa vizuri ...

GATUSO SASA HIZI SIFA

Image
Na Yego Sholla Maisha chini ya Gennaro Gattuso pale AC Milan yamebadilika sana. Matokeo yanaonekana kuja upande wao vizuri sana tofauti kabisa na matarajio akiwa ameiongoza timu hiyo mara 13 na kushinda 9 na sare 4 huku akiwa amekwenda zaidi ya dakika 500 bila kuishuhudia timu yake ikiruhusu bao pia. Lakini Kama kuna kitu ambacho kinamsaidia mbabe huyo wa soka kwenye uongozi wake pale AC Milan basi ni utu ama “Personality” yake kwa kimombo. Ni kweli alikuwa mkorofi enzi za uchezaji wake lakini ile picha imejenga heshima kubwa kutoka kwa wachezaji wake. Sio kwamba atampiga mtu kichwa pale atakapokosea! lakini anaondoa ile hali ya kujisikia na timu inacheza kwa ajili ya kulinda na pengine kurudisha sura ya timu yenyewe. Hata hamasa inakuwa kubwa na matokeo huwa yanatafutwa kibabe sana. Ignazio Abate sasa hivi hapati namba kisa ufaza. Kocha haitumi nafsi kufanya vile isivoweza lakini bidii iwepo na ujue mwalimu anataka nini. Hata Antoinne Griezmann mwanzoni aliona mambo magu...

ARSENE WENGER AWATUPIA LAWAMA WACHEZAJI WAKE

Image
Miaka 20 imepita, miaka yenye rangi mbali ndani ya maisha ya Arsene Wenger ndani ya kikosi cha Arsenal. Hapana shaka rangi nyeupe ilitanda katika ngozi ya mwili wake ndani ya miaka 10 ya kwanza. Miaka ambayo alifanikiwa kupata mafanikio makubwa katika soka la England. Mafanikio ambayo yalimpa heshima kubwa sana ambayo vizazi vingi vitaikumbuka. Ndiyo miaka kumi ambayo alifanikiwa kupata kushinda makombe matatu pekee aliyonayo ya ligi kuu ya England, kombe ambalo kwa sasa linaonekana gumu kwake kushinda tena. Hapana shaka nyakati hizi zenye majira ya ushindani na mapinduzi makubwa ndani ya mpira duniani hazitoi nafasi kwake yeye kushinda tena kombe hili. Upinzani mkubwa umeongezeka, mapinduzi ya uwekezaji mkubwa wa timu mbalimbali ndani ya uwanja yanafanyika kwa kiasi kikubwa ndiyo maana siyo jambo la kushangaza Manchester City imetoka kwenye kisigino mpaka kichwani. Mapinduzi ambayo yanaipa nafasi Chelsea kuwa timu ambayo ina mafanikio ...

Mafisango atawafanya Simba waisome historia ya Benfica na laana ya Guttman

Image
Na HAATIM ABDUL. Asubuhi ya Mei 22, 1990. Ni katika mji wa Vienna huko Austria. Anaonekana mwanaume mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti kwa unyenyekevu mkubwa, pembezoni kabisa mwa kaburi.  Macho ya mtu huyu yalikuwa yakitiririka machozi mithili ya mvua za rasha rasha. Machozi hayo yakidondokea sakafu ya ukingo wa kaburi hilo lililopo mbele yake. Huzuni ilioje! Ziara hii haikuwa ya kawaida. Ni ziara iliyojaa msisimko, msisimko wenye majuto ndani yake. Mtu huyu aliyepiga magoti asubuhi hii kaburini akiwaongoza wenzake si mwingine bali ni Eusebio Da Silva. Ndani ya kaburi hili, mwili wa aliyekuwa kocha wake wa zamani aliyeitwa Bela Guttman umelala ukiwa tayari umeoza. Bela hana kauli tena. Lilikuwa ni ombi la kufutiwa laana iliyoikumbuka klabu ya Benfica kabla ya kesho yake kupambana na Ac Milan katika fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Machozi ya Eusebio kwenye kaburi la Bela Guttman hayakuweza kusaidia lolote. Ni Mei 23,1990 katika dimba la Prater...

IJUE HISTORIA YA SOKA DUNIANI LEO :sehemu ya pili

Image
Uwanja :-               Uwanja una umbo la mstatili. Hakuna kipimo kamili, ila kanuni zinasema urefu ni baina ya mita 90 na 120, upana baina ya mita 45 na 90. Kwa michezo ya kimataifa urefu uwe baina ya mita 100 - 110 na upana baina ya mita 64 na 75. Goli ziko kwenye pande fupi zaidi. Kuna alama ya bendera kwenye kona za uwanja. Mwaka 2008 IFAB ilijaribu kusanifisha vipimo kuwa mita 105 kwa 68, lakini kanuni hii ilisimamishwa baadaye. Mstari ni mpaka wa uwanja. Wakati mpira uko kwenye mstari hata kwa kiasi kidogo unahesabiwa bado uko ndani ya uwanja. Kwa goli kukubaliwa sharti mpira uwe umepita mstari wa goli kabisa. Mpangilio wa wachezaji Kuna wachezaji wa aina tatu: walinzi, wachezaji wa kiungo na wachezaji wa mbele au straika. Goli kipa au mlinda lango ni mmoja kati ya walinzi. Ni uamuzi wa kocha kuhusu idadi ya wachezaji wa kulinda lango, wa kiungo au wa mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Mfumo wa 4-4-2 umekuwa maarufu miongoni mwa tim...

IJUE HISTORIA YA SOKA DUNIA LEO :sehemu ya kwanza

Image
Kwa msaada wa mtandao  Mpira wa miguu (pia soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja. Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kufunga goli, yaani kuuingiza mpira katika wavu wa wapinzani mara nyingi zaidi. Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya kutoka nje ya uwanja. Historia :-              Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia . Wachina , Wajapani , Wakorea na Waitalia , wote hao walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya enzi zetu. Wagiriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata hivyo, ni nchini Uingereza ambapo umbo la soka la kisasa lilianza kulipuka. Ilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la M...

HAPA WALIPOFIKIA RUVU SHOOTING WANAPASWA KUPEWA MOYO ZAIDI...

Image
WIKI iliyopita klabu ya Ruvu Shooting ilifanya hafla yake fupi ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya mambo kadhaa yaliyotangazwa mtandao wa kijamii wa facebook wa saleh Ally unasema kuwa Shooting walikuwa wamejipanga na mambo mengi ambayo yalionyesha wazi kwamba wana mipango endelevu na ya muda mrefu. Klabu hiyo ilitangaza rasmi kuingia katika mfumo wa hisa wakiindoa mikononi mwa jeshi na sasa wamiliki watakuwa ni wale walionunua hisa. Ingawa jeshi nalo lina hisa zake, lakini watu wengine kama akina Saleh Ally, nao wanaweza kuwa na nafasi ya kumiliki Ruvu Shooting, moja ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara. Maana yake, Ruvu Shooting wameamua kuingia katika mikono mchanganyiko, yaaniile ya jeshi pamoja na wadau wengine wa soka na kwa kiasi kikubwa itawaongezea idadi ya mashabiki ambao watafuta mawazo ya kuwa ni timu ya jeshi. Timu nyingi ambazo hujulikana kuwa ni timu za jeshi pekee, wananchi wamekuwa hawapendi kujihusisha nazo kwa kuwa wanaamini kwamba tayari zina wahusika wenyewe....

Mafanikio ya Msuva yanapogeuka changamoto kwa mdogo wake

Image
Taarifa kutoka mtandao wa Football Tanzania umeripoti kuwa James Msuva ni mdogo wake Simon Msuva ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Difaa el Jadida ya Morocco, james ni miongoni mwa wachezaji wa mbao ambao wanafanya vizuri kwa sasa tofauti na wakati alipojiunga na klabu hiyo ya Mwanza ambapo alikuwa anaanzia benchi lakini siku za hivi karibuni amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha kwanza. James ameelezea changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo kwenye soka la Tanzania ili kufikia malengo yake pengine hata pale alipofikia kaka yake. “Namshukuru Mungu toka nilipotoka hadi nilipo sasa hivi, kuna mabadiliko makubwa ambayo nimeyaona hususan nilivyojengwa kiakili na kimwili,  kumenibadilisha kwa namna moja ama nyingine kwa sababu ligi yetu ya Tanzania inachangamoto nyingi kama usipokuwa na utimamu wa mwili na akili huwezi kucheza.” “Namshukuru mwalimu wangu (Etiene Ndayiragije) na uongozi wa Mbao kwa kukiona kipaji changu na kukibadilisha, waliamini kwamba...

SINGIDA UNITED, ANZENI WALIOKOSEA MBEYA CITY

Image
Mapinduzi ya kizazi kipya cha watu kujivunia na kuzipenda timu zao za mikoani yalianzia kwa Mbeya City. Timu ambayo wana Mbeya walijivunia kuishabikia, kuipenda na kuisaidia kwa hali yoyote kadri ambavyo uwezo wao ulivyo waruhusu. Mbeya City hawakuwaangusha mashabiki wao mwanzoni, waliwapa furaha ambayo walitazamia kuipata kipindi ambacho wanaishabikia timu. Msimu wao wa kwanza kwenye ligi kuu walionesha ushindani wa hali ya juu, wakafanikiwa kuingia katikati ya wazee wawili wa mpira hala Tanzania ( Simba na Yanga) Kabla ya ligi kumalizika watu wengi waliipa nafasi Mbeya City kuchukua kombe, na hii ni kwa sababu ya matamanio ya watu wengi. Matamanio ambayo yalikuja kutokana na wao kuchoka kushuhudia kila siku Simba na Yanga wakibadilishana kombe la ligi kuu. Matamanio ambayo yaliifanya Mbeya City kupata mashabiki ambao hata siyo wazaliwa wa Mbeya, mtu wa Mwanza akawa anajivunia kuishabikia Mbeya City kwa sababu tu ya matokeo waliyokuwa wanayapata ndani ya uwanj...

ZANZIBAR WALIPATA FURAFA CECAFA, AIBU WAMEIPATA CAF.

Image
Tulishuhudia CECAFA, macho yetu yalipendezwa na vingi vilivyotokea Kenya kwenye michuano ya CECAFA. Furaha ambayo ilipitiliza kiasi kwamba tulitumia kubeza sehemu moja na kusifia sehemu nyingine bila kutuliza akili zetu kwa umakini. Zanzibar ilisifiwa sana, Tanzania bara ilizodolewa sana, cha ajabu tulifika sehemu ambayo ilitulazimu kusema Zanzibar wana misingi imara ya soka na kama wakipewa uanachama wa FIFA watafuzu kombe la dunia. Nilishtuka baada ya kusikia maneno hayo, nafsi yangu iliniambia usiingie kwenye mkumbo huo wa kusifia wakati nikiwa na furaha. Akili yangu ilitulia nikaamua kuandika makala ambayo niliwaambia Zanzibar maeneo wanayotakiwa kuyapitia ili na mimi niwasifie. Sikutaka kuwasifia Zanzibar na kuwaweka daraja la juu kwa sababu ya kufika kwao fainali ya kombe la CECAFA. Michuano ambayo haina ushindani na mvuto ndani na nje ya uwanja, michuano ambayo timu za taifa hupeleka vikosi vya vijana kushiriki michuano hiyo. Michuano ambayo Zanzibar ili...

MAHADHI WAKUMBUKE MAZEMBE UJIFUNGE MASOMBO

Image
Najua ushapitia nyakati tofauti zenye majira tofauti sana katika maisha yako, na kuna wakati mambo yako yalienda shoto na yakarudi upogo kwa sababu mbalimbali na kuna nyakati mambo yako yalitembea kwenye mstaari mnyoofu. Nyakati hizi zilikuwa na maana kubwa sana kwenye maisha yako kwa sababu maisha ya mwanadamu hukamilika kipindi ulimi wake unapoonja pilipili na asali. Maisha hayawezi kuitwa maisha kama yatakuwa na upande mmoja wa shilingi, ndiyo maana tunatakiwa tuwe dhabiti pindi kombo anapotutembelea sebuleni kwetu. Kuna wakati miguu yako ilikuwa mizito kwa kila hatua uliyokuwa unajaribu kupiga ili usogee kwenda mbele. Mbele yako hukuona mwangaza wowote, giza lilikuwa linatawala mboni zako za macho kiasi kilichopelekea wewe kutoiona njia sahihi uliyotakiwa kuifuata ili kufika ulipokuwa unatamani kupafikia kabla hujakanyaga jiji la Dar es Salaam. Jiji ambalo hutia upofu wa akili kipindi unapotanguliza kichwa kukanyaga ardhi yake na kuipa miguu jukumu la kuona ...