WAAMUZI WA KIINGEREZA KUTOWEPO URUSI.

Na Yego Sholla

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 80, nchi ya Uingereza haitakuwa na mwamuzi kwenye michuano ya kombe la dunia. Lakini ni UK nzima kwa maana ya Uwelshi, Uskochi, na Jamhuri ya Ireland. Lakini gumzo kubwa lipo Uingereza maana hata kiuwezo lenyewe ni taifa kubwa kimpira ukilinganisha na hayo mengine.

Wana ligi inayofuatiliwa zaidi na wamekuwa na kawaida ya kuamini kuwa ubora wote uko kwao pia. Promo na vitu kama hivyo na ndio maana kuna mshtuko miongoni mwa wengi kuwa hawana hata mwamuzi mmoja kwenye michuano hii.

Sababu ambayo wengi watakupa ni kwamba ubora wa waamuzi kutoka nchini humo umepungua. Hili linaweza kuwa kweli lakini hebu tuangalie vizuri na mengine.

Kikawaida mwamuzi huwa anasemekana kufikia kilele cha uamuzi pale anapofanikiwa kuchezesha fainali ya michuano mikubwa zaidi ya soka Ulimwenguni. Na hili huwa liko wazi kutokana na ubora wa mwamuzi husika kwenye kuchezesha soka la ngazi mbali mbali hapo kabla. Hivyo basi waamuzi kutoka Uingereza ndio wamechezesha michezo mingi zaidi ya fainali za kombe la dunia. Ambapo waamuzi kutoka nchini humo wamekwisha fanya hivyo mara 3. Ni taifa la Italy pekee ndio linafikia hii rekodi.

Ukitaka kuamini hili jaribu kuangalia hata waamuzi watatu maarufu zaidi duniani kwa karne ya karibuni wametoka nchi gani. Peraguia Collina kutoka Italy ambaye anasemekana na wengi kuwa mwamuzi bora wa muda wote kwenye soka, Huyu ndio pia aliechezesha fainali za kombe la dunia baina ya Brazil na Germany mwaka 2002. Akafuata Howard Webb ambaye ndie mwamuzi pekee kuwahi kuchezesha fainali ya klabu bingwa na ile ya kombe la dunia ndani ya mwaka mmoja na hiyo ilikuwa ni mwaka 2010.

Baada ya hapo Mark Clattenburg ambaye alichezesha pia mchezo wa fainali ya michuano ya Euro mwaka 2016 ndio alifuata na baada ya Webb huyu ndio alikuwa na amri zaidi nchini England na wasichokijua wengi ni kwamba huyu ndio alikuwa mwamuzi pekee aliechaguliwa kwa ajili ya fainali za kombe la dunia nchini Russia lakini kitendo cha yeye tayari kuwa na nyadhfa ya kuwa rais wa waamuzi nchini Saudi Arabia kilimnyima shavu hili. Shirikisho la soka nchini England,  FA kilipendekeza baadhi ya majina menginw kama mbadala lakini FIFA walikataa ombi lao.

Hapa utagundua kuwa sio kwamba England walikosa nafasi ya kupeleka waamuzi kutokana na ubora wao kushuka lakini kwa sababu baada ya Clattenburg, Uingereza haijakuwa na mwamuzi maarufu na mwenye consistency kubwa kama huyu. Sijui nimeeleweka? Kiufupi ni kwamba England wanazingatia sana ubora na heshima ya waamuzi wao na ndio maana si ajabu tangu Clattenburg atolewe Waingereza wenyewe hawapigii kelele swala hili.

Wanachohitaji Waingereza kwa sasa ni mwamuzi atakaeibuka na kuwa bora miongoni mwa hao waliopo na akaweza pia kuwa gumzo ulimwenguni kama ilivyokuwa kwa kina Webb na Clattenburg. Uingereza kama umeipeleleza vizuri imekuwa na kawaida ya kutoa mwamuzi mmoja tu hivi karibuni lakini ambaye anasifika ulimwenguni kote jambo ambalo kwa sasa halipo.

Howard Webb alikuwa mwamuzi kwenye mashindano mawili ya kombe la dunia mwaka 2010 na 2014 kwani huyu aliweza kuwa ndio mwamuzi bora sio tu Uingereza wakati huo bali hata duniani.  Na ukitaka kuamini hili wakusanye mashabiki kadhaa wa soka wataje mwamuzi au hata watatu tu wanaowajua basi jina la Webb haliwezi kukosa hata sasa licha ya kuwa amestaafu na ni askari polisi.

Huyu ni mwamuzi ambae alishathibitisha ubora wake na mamlaka makini alionayo kwenye uamuzi pale Uingereza na si ajabu ndio mwamuzi pekee kwenye historia kuchezesha fainali mbili kubwa ndani ya mwaka mmoja. Unadhani heshima hii inakwenda kwa nani kama sio Waingereza wenyewe hao tunaowacheka kuwa hawana mwamuzi hata mmoja Urusi.

Michuano ya Euro 2016 mwamuzi kutoka England alikuwa pia ni mmoja tu, Mark Clattenburg na ndie aliechezesha pia mchezo wa fainali na kuchora tattoo kwenye mkono wake. Huyu pia amewahi kuchezesha fainali mbili ndani ya wiki moja, ya FA na klabu bingwa.

Na kwa ujumla ukifuatilia vizuri utagundua kuwa Waingereza wamekuwa hawana kawaida ya kutoa waamuzi wengi kwenye michuano mikubwa lakini ubora kwao ndio umekuwa kipaumbele na haishangazi kuwa yenyewe ndio ina waamuzi waliochezesha fainali nyingi zaidi za kimataifa kwenye miaka 8 iliopita. Kwa sasa anaesubiriwa ni mrithi tu wa Clattenburg. Kwaiyo pengine sio ubora kupungua kama wanavyodhani wengi lakini pengine yule wa kulinda sifa bora ya waamuzi kutoka nchini humo hajapatikana.

Kwa miaka takribani 18 iliopita waamuzi bora na maarufu zaidi wametoka nchi mbili pekee, Italy na Engalnd. Ni wazi wanapaswa kuilinda sifa hii. Wazungu huwa wanasema, "Quality is better than Quantity".Credit Haatim Abdul

Comments

Popular posts from this blog