Posts

Showing posts with the label Simba

JUA KWANINI NIYONZIMA ASEMAYANGA HAIMTISHI WALA HAIMPI HOFU NA KUIPONGEZA SIMBA

Image
Na Joseph michael Haruna niyonzima mchezaji wa SIMBA lakini kabla ya hapo alikuwa akiichezea timu pinzani ya SIMBA yani YANGA ambako mwanzoni mwa msimu huu wa 2017/2018 Niyonzima alihamia SIMBA.Pamoja na kuanza msimu kwa kiwango kisicho ridhisha akiwa SIMBA Haruna Niyonzima pia alikuwa nnje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia. Lakini habari njeema kwa mashabiki na wapenzi wa SIMBA ni kwamba Niyonzima amerudi uwanjani na ameanza kufanya mazoezi na timu na pia si ajabu tukashuhudia akiecheza mechi ya SIMBA NA NJOMBE MJI ambayo itachezewa mjini njombe. Baaada ya kufanya mahojiano na CLOUDS FM jana Niyozima alizungumzia mambo mengi sana pamoja na kuelezea hali yake ya kiafya kuimarika vizuri na kuwa teyari kuingia uwanjani japo kuwa alikumbusha kwamba kuhusu maelekezo au nafasi ya kucheza bahado yanategemea sana namna ambavyo mwalimu atapanga mipango yake na daktari wa timu atakavyo elekeza au shauri.Na pia hakusita kuipongeza timu yake ya SIMBA kwa kufanya vizuri kwenye ligi h...

SIMBA YATIMKIA IRINGA, WANNE WATAKAOIKOSA NJOMBE MJI HAWA HAPA

Image
Kikosi cha Simba Sc kinatarajiwa kuondoka Jijini Dar es salaam kesho Jumamosi ya March 31  kwenda Iringa, kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 2, katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji FC. Simba SC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC April 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Saba Saba-Njombe, huku mchezo huu ukitarajiwa kupigwa majira ya saa 16:00 jioni. Kuelekea mchezo huo Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara amesema kwamba Simba itakuwa Iringa kuanzia kesho Jumamosi hadi Jumatatu mapema itakaposafiri kwenda Njombe. “Timu itasafiri kwenda Njombe Jumamosi hii kupitia Iringa ambako itaweka kambi hadi Jumatatu, kabla ya mechi ya Jumanne ya Aprili 3.  “Tunaamini tutashinda inshaallah, muhimu dua na sala zenu. Mtupokee nyanda za juu kusini mwa Tanzania,”amesema Manara. Katika mchezo huo, Simba SC itamkosa kiungo wake tegemeo wa kati, Jonas Mkude ambaye aliumia kifundo cha mguu wiki hii katika mazoezi yaliyokuwa yanafanyika kwenye Uwanja wa Boko...

HII HAPA RATIBA KAMILI YA SIMBA SC MICHEZO 10 IILIYOBAKI MSIMU HUU

Image
HII HAPA RATIBA KAMILI YA SIMBA SC MICHEZO 10 IILIYOBAKI MSIMU HUU 1:April 03-2018, Njombe Mji itaikaribisha Simba Sc saa 16:00 kwenye uwanja wa Sabasaba-Njombe 2:April 09-2018, Mtibwa Sugar wataikaribisha Simba Sc saa 16:00 kwenye uwanja wa Jamhuri-Morogoro 3:April 12-2018, Simba Sc wataikaribisha Mbeya City saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam 4:April 16-2018, Simba Sc wataikaribisha Tanzania Prisons saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam 5:April 20-2018, Lipuli Fc wataikaribisba Simba Sc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Samora-Iringa 6:April 29-2018, Simba Sc wataikaribisha Young Africans saa 16:00 kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam 7:May 06-2018, Simba Sc wataikaribisha Ndanda Fc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam 8:May 13-2018, Singida United wataikaribisha Simba Sc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Namfua-Singida 9:May 19-2018, Simba Sc wataikaribisha Kagera Sugar saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Uhuru-Dar es ...

WATANO WALIOKUWA STARS KUONGEZA NGUVU SIMBA

Image
Wachezaji watano wa Simba waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba mud wowote kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji. Simba inaendelea kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji Aprili 3 mwaka huu, mchezo ambao ni kiporo. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya, Aishi Manula, Shomari Kapombe,Erasto Nyoni na Said Ndemla. Kikosi cha Simba kiliendelea na mazoezi hapo jana jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterani, katika maandalizi ya mchezo huo wa ligi kuu Tanzania Bara.

MANARA AMFANANISHA SHIZA KICHUYA NA MESSI (LA PULGA)

Image
Nyota wa Simba Sc, Shiza Ramadhan Kichuya aliyeonesha ubora wake jana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya DR Congo ametajwa kuwa ni Messi wa Tanzania. Kichuya alifanikiwa kufunga goli la pili na kutoa pasi ya goli la Kwanza katika ushindi wa goli 2-0 kwenye uwanja wa Taifa Jijni Dar es salaam. Baada ya mchezo huo kuisha Afisa Habari wa Simba Haji Manara alielezea kwa ufupi sana akisema ni dhambi kumfananisha Kichuya na La Pulga (Lionel Messi) lakini kibongo bongo Kichuya ni Messi wa Tanzania. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara aliandika hivi: "Sitaki kumfananisha na La Pulga..kwangu ni dhambi kuu isiyohitaji msamaha hata wa Shetani..ila kwa vwango vya kibongo bongo huyu ndio La Pulga wetu..kitu kinachowafananisha ni kufunga na kuassist..halaf anafunga ktk game kubwa..nadhani tunaelewana vzuri hapo hususan wale wabishi wabishi..nakuletea kdogo tu goli za Tanzanian la pulga kichuya na miassist yake kama mvua" @kichuya_ 👏👏🙌.

SIMBA WAZUNGUMZIA MAENDELO YA JONAS MKUDE

Image
Kiungo mkabaji wa Simba Sc, Jonas Mkude ambaye juzi aliumia mazoezini na kuibua hofu kwa wanamsimbazi, anatarajiwa kurejea mazoezini kesho. Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema baada ya kufanyiwa vipimo, imebainika kuwa Mkude alipata majeraha ya michubuko ya kawaida. Amesema hakuna wasiwasi juu ya afya yake na atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachotarajiwa kusafiri kwenda mkoani Njombe kuivaa Njombe Mji April 03. Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi hapo jana kwenye uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo. Wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa wanatarajiwa kujiunga na wenzao muda wowote baada ya kukamilika kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Tanzania dhidi ya DR Congo. Katika mchezo huo Tanzania ilifanikiwa kuibika na ushindi wa magoli 2-0 mchezo uliofanyika katika  uwanja wa Taifa, huku Shiza Kichuya akin'gara katika mchezo huo kwa kufunga bao moja na kutengeneza jingine lililofungwa na Nahodha Mbwana Ally Samatta.

NIYONZIMA, MBONDE MAMBO SAFI SIMBA SC

Image
Wakati Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba Sc wakiwa na mechi 10 mbele kabla ya msimu kuisha mambo yanaonekana kwenda sawa baada ya wachezaji wao waliokuwa majeruhi kurejea. Katika mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa Boko kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Njombe, beki wa kati aliyepata ajali ya pikipiki siku chache zilizopita Salim Mbonde ameanza mazoezi na wenzake. Hata hivyo, Mbonde amekuwa akizunguka uwanja pembeni ili kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya kuungana na wenzake. Pamoja na Mbonde, habari njema nyingine ni kuwa kiungo aliyetua Msimbazi akitoea kwa watani wao wa Jadi Yanga Sc, Haruna Niyonzima, naye ameanza mazoezi ya uwanjani. Niyonzima alipata majeraha katika mazoezi, yaliyompelekea kusafiri hadi India ambako alipatiwa matibabu katika mguu wake, na sasa ameanza mazoezi ya uwanjani lakini kwa kuzunguka pembeni ya uwanja. Kabla ya hapa Niyonzima alisema kuwa 'Kwa sasa anajisikia nafuu na ameanza kupewa ratiba na mwalimu pia anamini mambo yatakuwa mazuri...

RIPOTI YA DAKTARI WA SIMBA KUHUSU MKUDE BAADA YA KUUMIA MAZOEZINI

Image
Kiungo wa Simba Sc, Jonas Gerald Mkude ameumia kifundo cha mguu wa kulia (Ankle) akiwa mazoezini leo jioni Jumatatu ya March 26-2018. Baada ya kutolewa nje ya uwanja na kupatiwa huduma ya kwanza uongozi wa Simba kupitia  ukurasa wao wa Instagram umesema  kuwa umeongea na Daktari wa Simba  Bwana Yassin Gembe kuhusu majeraha hayo aliyoyapata Mkude. 'Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali na si majeraha makubwa sana, ila kesho (leo) ndio tutatoa taarifa kamili kuhusianana na hali yake kwa ujumla ila kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia' amesema Bwana Yassin Gembe. Simba inaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veteran, katika kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji April 03 mwaka huu kwenye uwanja wa Sabasaba

HARUNA NIYONZIMA MAMBO NI MAGUMU SANA

Image
Na Yego Sholla 'Kwa sasa najisikia nafuu na nimeanza kupewa ratiba na mwalimu naamini mambo yatakuwa mazuri. Kuna ‘recover’ za aina mbili kuna ya daktari na mwalimu, ya daktari tayari nimeshafanya sasa hivi nafanya ya mwalimu kwa hiyo ikiisha najiunga na timu.”taarifa kutoka mtandao wa Shafih daud “Nimemi-miss kucheza kwa sababu muda mrefu sijacheza na watu wanajua mpira ni kazi yangu lakini siwezi kuchukua uamuzi nikasema nacheza, natakiwa kwenda na ratiba ya timu, daktari na mwalimu lakini sasa hivi nipo kwenye ratiba ya mwalimu, muda si mrefu nitarudi uwanjani.” HARUNA NIYONZIMA

HIVI NDIVYO HARUNA NIYONZIMA ALIVYO REJEA MSIMBAZI KWA MKWARA MZITO

Image
Na Yego Sholla Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima amerudi katika kikosi cha Simba SC baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Niyonzima alikwenda india kwa ajili ya matibabu ambapo ilielezwa angefanyiwa upasuaji mdogo lakini jambo zuri ni kwamba alitibiwa bila kufanyiwa upasuaji. Niyonzima anaamini baada ya muda mfupi atarudi uwanjani baada ya kumaliza ratiba ya mwalimu. Siwezi kuja mazoezini kabla sijawa vizuri, lakini siwezi kusema nipo vizuri kwa 100% watu wanachotakiwa kujua, mtu ukitoka kwenye maumivu huwezi kuja kujiunga na timu moja kwa moja lakini ninachoshukuru naona kama napiga hatua kwa sababu siku za nyuma nilikuwa nyumbani lakini sasa nimeanza kuungana na timu.” “Kwa sasa najisikia nafuu na nimeanza kupewa ratiba na mwalimu naamini mambo yatakuwa mazuri. Kuna kupona kwa aina mbili kuna ya daktari na mwalimu, ya daktari tayari nimeshafanya sasa hivi nafanya ya mwalimu kwa hiyo ikiisha najiunga na timu.” “Natamani kucheza kwa sababu muda mrefu sijacheza ...

SIMBA VS YANGA KUPIGWA TAREHE HII

Image
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi Simba na Yanga watacheza. Timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo. Awali Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati.

SIMBA SC: HABARI MPYA LEO JUMATATU YA MARCH 26-2018

Image
Kikosi cha Simba jana Jumapili ya March 25-2018, kiliendelea kujifua kwenye uwanja wa Boko Veterani Jijini Dar es salaam katika kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji April 03 mwaka huu. Katika mazoezi hayo Simba inawakosa baadhi ya wachezaji walioko kwenye majukumu ya timu za Taifa. Wachezaji hao ni Emanuel Okwi, Juuko Murshid , Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Shiza Kichuya ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa. Wachezaji hao wanatarajia kurejea kikosini mapema wiki hii baada ya michezo ya kirafiki ya mataifa yao hapo kesho. Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafika na DR Congo kesho Jumanne ya March 27, huku Uganda ikitarajiwa kucheza na Malawi. Kuelekea mchezo huo na Njombe Mji, timu ya Njombe Mji imeelezea kutoridhishwa na maamuzi ya uongozi wa TFF kwa sababu ratiba inakuwa imewabana sana. Ratiba ya Njombe Mji iko kama unavyoona hapa chini Stand United vs Njombe Mji (Machi 30-2018) Kambarage Stadium Shin...

"MO" DEWJI ATENGA MAMILIONI YA PESA KWA KILA MECHI SIMBA

Image
Mwanachama na shabiki wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ub­ingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifaniki­sha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100. Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara, alisema: “Huu ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu kuipambania timu yao kutwaa ub­ingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma. “Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo. “Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuonge­za hamasa kwa wache­zaji,” alisem...

SIMBA WATENGA MECHI 5 ZA UBINGWA

Image
Kwa mujibu wa benchi la ufundi la Simba, wametenga mechi 5 ambazo zimebeba pointi zitakazowapa ubingwa. Simba inayonolewa na Mfaransa Pierre Lechantre kwa sasa ndiyo inaongoza katika chati ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 46, sawa na Yanga ambao nao wana idadi hiyo ya pointi. Kikosi hicho katika michezo hiyo 10 yenye pointi 30 mechi tano watazichezea katika Uwanja wa Taifa huku tano wakizicheza mikoani. Mechi ambazo Simba watafuata pointi mkoani ni pamoja na Majimaji ya Songea, Lipuli FC ya Iringa, Singida United ya Singida, Njombe Mji ya Njombe na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kocha msaidizi wa kikosi hicho, Masoud Djuma raia wa Burundi amesema; “Tunatakiwa kuweka malengo ya kupata pointi kwenye mechi zote za mikoani.” Kama Simba watafanikiwa kupata ushindi katika michezo yote hiyo watavuna pointi 30 ambazo ukijumlisha na 46 ambazo wanazo sasa watafikisha pointi 76 zitakazokua 3 mbele ya Yanga watakaomaliza ligi wakiwa na 73.

OKWI, BOCCO, KICHUYA WATENGEWA MILIONI 100, ISHU KAMILI IKO HIVI

Image
Mabosi wa Simba wajanja sana. Jamaa hao wana akili sana na kwa kuwa hawataki kupishana tena na taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara, wamewatengea fungu la maana nyota wake Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya ili kuwapa mzuka Bara. Mabosi wa Simba wameamua kuwatengea nyota wake hao kiasi cha Sh100 milioni ili kuhakikisha wanaweka rekodi ya kuvunja mwiko wa kukaa kwa muda bila kubeba taji la Ligi Kuu Bara. Simba ina msimu wa tano sasa ihaijabeba ndoo ya VPL. Mara ya mwisho kubeba taji hilo ilikuwa msimu wa 2011-2012 wakati huo Jonas Mkude akiwa kinda ndani ya kikosi hicho akitokea kupandishwa timu ya Vijana U20. Kama mnavyojua, Simba ndio kinara wa Ligi Kuu kwa sasa ikiwa na alama 46 sawa na Yanga, ila uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa unaibeba mbali na mechi mbili mkononi dhidi ya moja ya watani zao wakati ligi ikiwa raundi ya 22. Simba itaanza kula viporo vyake Aprili 3 kwa kuvaana na Njombe Mji kabla ya kusubiri kuvaana na Mtibwa Sugar ambao pia wana kiporo na Yanga. ...

OKWI, BOCCO WAAPA SIMBA BINGWA

Image
Baada ya Simba kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika, mastraika wa timu hiyo John Bocco na Emmanuel Okwi kwa pamoja wameapa kufia uwanjani ili Wekundu wa Msimbazi wabebe ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu. Simba iliondolewa na Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam halafu ugenini wakatoka suluhu. Kutokana na hali hiyo, Okwi na Bocco wamesema lengo lao sasa ni kuhakikisha wanapambana kufa na kupona kwenye Ligi Kuu Bara ili waweze kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa. Simba inaongoza katika ligi kuu ikiwa na pointi 46 sawa na Yanga, inayoshika nafasi ya pili, lakini wenyewe wana tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa. Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi alisema, mipango yao ya kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho imekwama, sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi kuu. “Tunarudi kujipanga kwenye ligi kuu, kwani ndiyo sehemu pekee tunapotakiwa tupambane kufa na kupona ili mwakani tuwez...

HIKI NDICHO KIASI ANACHOKATWA MCHEZAJI WA SIMBA ANAYECHELEWA KULA

Image
Uongozi wa benchi la ufundi la Simba umeweka sheria kali ambapo kila mchezaji akichelewa kwenye matukio maalum anakatwa shilingi laki moja. Uongozi huo chini ya kocha Pierre Lechantre umeweka sheria hiyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inakuwa na nidhamu ya hali ya juu. Sheria hiyo ya Simba inasema kuwa kama mchezaji akichelewa kula, akichelewa mazoezini, akichelewa kwenye basi na sehemu nyingine muhimu anakatwa kiwango hicho cha fedha. “Huu ni utaratibu wetu kwa muda mrefu kidogo kuanzia benchi hili la ufundi limeanza kazi. “Wachezaji wanatakiwa kuwahi sehemu zote muhimu, kila sehemu hata Ulaya wachezaji wanatakiwa kula pamoja, wanatakiwa kuwahi kwenye basi na mazoezini. “Utaratibu huu umeleta nidhamu ya hali ya juu klabuni, ndiyo maana umeona timu inafanikiwa kwa sasa kwa kuwa kuna nidhamu ya hali ya juu sana kwa sasa. “Kama kwenye chakula na sehemu nyingine kocha ndiye amekuwa akimwita meneja na kumwambia mkate mchezaji fulani shilingi 100,000, hii ni faida kubw...

KAULI YA KOCHA MSAIDIZI, SIMBA IKIANZA KUIWINDA NJOMBE MJI

Image
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema watautumia vyema muda ambao timu hiyo haina mechi za kimataifa na Kombe la FA kurekebisha makosa ya kiufundi waliyoyabaini ili warejee kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na kasi. Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi leo Jumamosi ya March 24-2018, kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa Aprili 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Saba Saba mkoani Njombe. Djuma, amesema wanataka kuona hawapotezi pointi katika mechi zao zote zilizobaki ili kutimiza mipango yao ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu. Djuma amesema wana lengo la kukiimarisha zaidi kikosi chao kwa sababu hatua iliyobaki ni ngumu zaidi kutokana na vita ya kuwania ubingwa na ile ya kushuka daraja kufanana. "Tunaelekea mwisho wa ligi, huku ni kugumu zaidi na ndio tunahitaji kushinda, ukipoteza pointi, basi umempa nafasi mpinzani wako, hatutaki kuona tunapoteza hii nafasi iliyobaki ya kushinda taji msimu huu,". Djuma al...

HABARI NJEMA KUHUSU BEKI WA SIMBA SC SALIM MBONDE

Image
Hivi karibuni beki wa Simba Sc aliyetua Simba kutokea Mtibwa Sugar, Salim Mbonde alipata ajali ya pikipiki iliyomsababishia majeraha juu ya jicho na kushonwa nyuzi tatu. Ajali hiyo ilisababisha beki huyo aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar aondolewe kwenye kikosi cha Simba kilichosafiri kwenda nchini Misri. Taarifa za uhakika ni kwamba beki huyo ameondolewa nyuzi alizoshonwa na sasa yuko tayari kurejea mazoezi ya kikosi cha Simba kuanzia Jumatatu ijayo. Alipotafutwa Salim Mbonde alisema kuwa Kwa sasa yuko fiti, na anataarajia kuungana na kikosi cha wenzake hapo Jumatatu ya wiki ijayo kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara unaofuata dhidi ya dhidi ya Njombe. Simba inatarajiwa kuivaa Njombe Mji April 03 mwaka huu, katika mchezo ambao ni kiporo baada ya Simba kushiriki michuano ya kimataifa kabla ya kutolewa na Al Masry ya nchini Misri.

VIPORO VYA SIMBA SASA NI WAZI TAREHE KAMILI HIZI HAPA

Image
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Njombe Mji na Simba SC uliokuwa umeahirishwa, sasa umepangwa kufanyika tarehe 3, Aprili mwaka huu, katika dimba la Sabasaba mjini Njombe. Awali kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Machi 11 mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuipa Simba nafasi ya kufanya maandalizi ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Al Masry katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Taarifa kutoka ndani ya Bodi ya Ligi zimethibitisha tarehe hiyo, na kueleza kuwa tayari timu zote mbili zimekwishapata taarifa kwaajili ya maandalizi. Aidha 8 April 2018 kikosi cha Simba kitashuka tena uwanjani dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro