WATANO WALIOKUWA STARS KUONGEZA NGUVU SIMBA

Wachezaji watano wa Simba waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba mud wowote kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji.

Simba inaendelea kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji Aprili 3 mwaka huu, mchezo ambao ni kiporo.

Wachezaji hao ni Shiza Kichuya, Aishi Manula, Shomari Kapombe,Erasto Nyoni na Said Ndemla.

Kikosi cha Simba kiliendelea na mazoezi hapo jana jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterani, katika maandalizi ya mchezo huo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Comments

Popular posts from this blog

Njia sahihi za kuachana na unywaji wa pombe