Posts

Showing posts with the label Tetesi

BARCELONA WAMETHIBITISHA KUFANYA MAWINDO YA KUMUWINDA ISSA DIOP

Image
Na Yego Sholla Barcelona wamefanya mawasiliano na klabu ya Toulouse kuhusu usajili wa beki wao Issa Diop, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sport. Barcelona wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu beki huyo kwa miaka kadhaa na wiki iliyopita wamewasiliana na kambi yake ili kujua mustakabali wake. Akithaminishwa kwa kiasi cha Euro Muilioni 25 beki huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akiwindwa na vilabu kadhaa barani Ulaya. Kama Barca wataamua kumsajili au La , majira ya kiangazi itategemea kama beki Samuel Umtiti  atasaini mkataba mpya  na Thomas Vermaelen  ataamua kubaki Camp Nou. Vinara hao wa La Liga pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Schalke ya Ujerumani, Thilo Kehrer. Beki huyo mwenye umri wa miaka 21 mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

PARIS SAINT-GERMAIN :WAMTOLEA JICHO MIRALEM PJANIC

Image
Na Yego Sholla Paris Saint-Germain wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Juventus  Miralem Pjanic, kwa mujibu wa taarifa kutoka  Corriere della Sera. Vinara wa Ligi kuu ya Ufaransa wameweka mezani ofa ya mkataba wa miaka  mitano wenye thamani ya Pauni Milioni 7 baada ya kodi kwa mwaka , mara mbili ya ile anayolipwa Juve kwa sasa ya Pauni Milioni 3.9

JOSEE MOURINHO :LUKE SHAW WEWE SEPA TU

Image
Na Yego Sholla Kocha wa Manchester United  Jose Mourihno imeripotiwa yupo mbioni kumsajili beki wa klabu ya juventus Alex Sandro ili kuja kuchukua nafasi ya Luke Shaw ambae amemwambia atafute mahali pa kwenda. #Www.nijuzehabari.co.tz update#

JOSE MOURINHO :WILLIAN €60 ITAPENDEZA ZAIDI

Image
Na Yego Sholla Kocha wa Manchester United yupo mbioni kumsajili Willian na tayari ametenga kiasi cha £60m kwa ajili ya nyota huyo mara msimu wa Ligi kuu utakapomalizika.

ANDERSON TALISCA KUTIMUKIA MANCHESTER UNITED

Image
Na Yego Sholla Manchester United inadaiwa kutenga kitita kwaajili ya kusaka saini ya kiungo wa Benfica Anderson Talisca. United bado haijaridhika na safu yake ya kiungo na imevutiwa sana Talisca anayeng’ara kwa mkopo huko Uturuki na timu ya Besiktas. Gazeti la A Bola la Ureno limedai kiungo huyo wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 24 ananukia kutua United na kwamba tayari maongezi baina ya pande zote mbili yamefika pazuri. Benfica inataka pauni milioni 35.5 ili kumwachia nyota huyo aliyefunga magoli 10 katika mechi 24 msimu huu.

JOSE MOURINHO AMTOLEA MACHO BEKI WA BARCELONA SAMUEL UMTITI

Image
Na Yego Sholla Manchester United wamekuwa wakifanya vikao kadhaa na wakala wa beki wa Barcelona , Samuel Umtiti, kwa mujibu wa taarifa kutoka Jarida la Michezo la nchini Hispania, Sport. Jose Mourinho anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa usajili wa beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye amejiimarisha kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya Barcelona tangu alipohamia hapo kutoka Lyon mwaka 2016. Jaribu la United la kumsajili Umtiti mwezi Januari mwaka huu ligonga mwamba na wapo tayari kutengua kipengele chake cha thamani ya Euro Milioni 60 iliyopo kwenye mkataba wake. Kwa mujibu wa Sport, United wamekuwa wakimfuatilia Umtiti kwa karibu sana na wameshafanya vikao kadhaa na kaka yake , Yannick Umtiti.

JACK WILSHERE AC MILAN WAMTOLEA MACHO SASA ARSENE WENGER KAZI IPO

Image
Na Yego Sholla Kiungo wa klabu ya Arsenal,  Jack Wilshere anawindwa na klabu ya AC Milan kuelekea dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sunday Express. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu , na siku ya Alhamisi alikuwa dimbani  San Siro  ndani ya uzi wa Gunners wakipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Milan , kombe la Europa. Wilshere mwenye umri wa miaka 26, anakusanya mshahara wa Pauni 120,000 ndani ya Emirates  ameambiwa mshahara wake upunguzwe kwa asilimia 25 na Gunners kitu ambacho amekataa na yupo huru kuongea na klabu yoyote ya nje ya Uingereza .

LEO MARCH 09 TETESI ZA SOKA NA USAJILI ULAYA

Image
Na Yego Sholla Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, mwenye umri wa miaka 24 ameamua kusalia katika klabu ya Tottenham kwa zaidi ya msimu mmoja lakini timu hiyo bado inakabiliana na ugumu wa kumbakiza mlinzi wa kati raia wa Ubelgiji Alderweireld, na mlinzi wa kushoto Danny Rose, ambao wote wanawaniwa na Manchester United. Kane anatarajiwa kuwa nahodha wa timu ya Uingereza katika michuano ya kombe la dunia akishirikiana na Jordan Henderson pamoja na Gary Cahill. Miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain inamtaka Antonio Conte kuwa meneja wao. Vinara hao wa The Ligue 1 wanamnyatia pia meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino. Mabosi wa Manchester United wanamuunga mkono meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho na watawapiga bei wachezaji wote wasioendana na mfumo wa mreno huyo. Klabu za Chelsea na Real Madrid zinaongoza mbio za kumuwania mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski raia wa Poland mwenye miaka ya 29 ambaye yuko mguu ndani mguu nje. Klabu ya Chelsea inapewa ...

HERRY KANE BADO NIPO NIPO SANA TOTTENHAM MWAKA MMOJA

Image
Na Yego Sholla Taarifa kutoka The Sun zinasema Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane, ameahidi kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya msimu mmoja, licha ya kusalia kwake, uongozi wa Tottenham unapambana kumbakiza kikosini beki wake Toby Alderweireld pamoja na beki wa kushoto, Danny Rose, wanaowania na Manchester United.

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI MARCH 04

Image
Manchester City watamenyana na mahasimu Manchester United na Tottenham kumsainia beki wa Fulham kijana wa miaka 17 Ryan Sessegnon. (Sunday Meneja wa West Brom Alan Pardew yuko kwenye hatari ya kupoteza kazi yake baada ya kipigo cha Jumamosi kutoka Watford. (Sunday Telegraph) West Brom wanajiandaa na kuondoka kwa wachezaji wengi ikiwa watashuka katika jedwali ambapo mlinzi wa Northern Ireland Jonny Evans, 30, kipa wa England Ben Foster, 34, mlinzi wa England Craig Dawson, 27, na msambulizi wa England Jay Rodriguez, 28, ambao wote wanavutia vilabu vingine. (Sun on Sunday) Meneja mjerumani Joachim Low anaibuka kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail on Sunday) Arsenal na Chelsea watang'ang'ana kupata huduma zake Carlo Ancelotti kama meneja mwisho wa msimu. (Sunday Express) Arsenal wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27, wakati klabu hiyo inataka kuzuia kumpoteza bila kunufaika msimu wa joto mwaka 2019....

Mario Lemina huyo Liverpool

Image
Liverpool wanajiandaa kuibomoa Southampton kwa mara nyingine tena kwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Gabon ,Mario Lemina majira ya kiangazi kwa mujibu wa taarifa kutoka L'Equipe. Lemina mwenye umri wa miaka 24 alitua katika dimba la St Mary's akitokea Juventus majira ya kiangazi yaliyopita  na ameonyesha kiwango kizuri katika msimu mbaya wa Southampton.

Griezmann nakwenda Barcelona

Image
Taarifa za hivi punde kutoka Sky Sports na Ulimwengu wa soka Tz zinasema  mwendo huu nadhani Uongozi wa klabu ya Barcelona utazidi kuongeza kasi ya kumsajili straika wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid. Mwanaume amefunga magoli saba katika mechi mbili zilizopita , baada ya hapo jana kuwatungua Leganes magoli manne peke yake na Jumapili aliwatungua Sevilla magoli matatu peke yake. Na hatimaye ameiwezesha timu yake kupunguza pointi dhidi ya vinara Barcelona na kuwa 4 , huku Barcelona wakicheza mechi yao moja ya mkononi usiku wa leo dhidi ya Las Palmas ,na siku ya Jumapili vilabu hivyo viwili ( Barcelona Vs Atletico Madrid ) vitashindana ubavu katika dimba la Nou Camp.

Tatizo sio pesa Liverpool bado hawajakata tamaa kwa JORGINHO

Image
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Star na Daily Mirror pamoja na Ulimwengu wa soka Tz Liverpool wamejitosa kwenye mbio za kunasa saini ya kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Star. Jorginho, kiungo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 26 ana mkataba na vinara wa Serie A mpaka mwaka 2020. Wiki iliyopita taarifa kutoka Italia ziliarifu kwamba Mabingwa wa Serie A , Juventus na Manchester United wanapigana vikumbo kuwania saini ya kiungo huyo na sasa Liverpool nao wamejiunga katika vita hiyo.

Simeone bado anamtaka AG7

Image
Taarifa kutoka Ulimwengu wa soka Tz zinasema kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone anawapa presha mabosi wa klabu hiyo kuhakikisha kwamba  Antoine Griezmann haondoki klabuni, kwa mujibu wa taarifa kutoka Mundo Deportivo. Taarifa zilizotoka wiki iliyopita kutoka Hispania zimedai kwamba Barcelona wanatarajiwa kutoa ofa ya Euro Milioni 100 kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwishoni mwa msimu huu. Griezmann ni mchezaji mkubwa ndani ya Atletico na Simeone anawataka mabosi wa klabu kufanya mazungumzo ya mkataba mpya ili kumzuia kuondoka na kutua timu nyingine msimu ujao.

Arsene Wenger ndo basi

Image
Uongozi wa klabu ya Arsenal, huenda ukafanya mabadiliko katika benchi la ufundi mwishoni mwa msimu huu, endapo hautoridhishwa na kazi ya  Arsene Wenger ambaye mwishoni mwa msimu uliopita alisaini mkataba mpya wa miaka miwili Gazeti la The Independent pamoja na the Sun yameripoti na kupitia tovuti mbalimbali za Michezo hapa Tanzania nazo zimeripoti  Uongozi wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, umepanga kufanya tathimini ya kina kuhusu mwenenndo wa mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, baada ya kuona hali sio nzuri katika kikosi chao msimu huu. Taarifa iliyochapishwa na kwenye gazeti la Daily Mail ya nchini England, imeeleza kuwa, uongozi wa The Gunners haukutarajia matokeo yanayopatikana hivi sasa, kufuatia imani kubwa waliyoiweka kwa babu huyo aliyedumu kwa kipindi cha miaka 20 tangu alipoajiriwa klabuni hapo. Taaifa hiyo imeongeza kuwa, The Gunners tayari wameshaanza kuandaa orodha ya makocha wa kuwatathmini katika kumpata mbadala wa Wenger kama itaamua kuachan...