BARCELONA WAMETHIBITISHA KUFANYA MAWINDO YA KUMUWINDA ISSA DIOP

Na Yego Sholla

Barcelona wamefanya mawasiliano na klabu ya Toulouse kuhusu usajili wa beki wao Issa Diop, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sport.

Barcelona wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu beki huyo kwa miaka kadhaa na wiki iliyopita wamewasiliana na kambi yake ili kujua mustakabali wake.

Akithaminishwa kwa kiasi cha Euro Muilioni 25 beki huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akiwindwa na vilabu kadhaa barani Ulaya.

Kama Barca wataamua kumsajili au La , majira ya kiangazi itategemea kama beki Samuel Umtiti  atasaini mkataba mpya  na Thomas Vermaelen  ataamua kubaki Camp Nou.

Vinara hao wa La Liga pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Schalke ya Ujerumani, Thilo Kehrer. Beki huyo mwenye umri wa miaka 21 mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog