Tatizo sio pesa Liverpool bado hawajakata tamaa kwa JORGINHO

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Star na Daily Mirror pamoja na Ulimwengu wa soka Tz Liverpool wamejitosa kwenye mbio za kunasa saini ya kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Star.

Jorginho, kiungo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 26 ana mkataba na vinara wa Serie A mpaka mwaka 2020.

Wiki iliyopita taarifa kutoka Italia ziliarifu kwamba Mabingwa wa Serie A , Juventus na Manchester United wanapigana vikumbo kuwania saini ya kiungo huyo na sasa Liverpool nao wamejiunga katika vita hiyo.

Comments

Popular posts from this blog