Simeone bado anamtaka AG7

Taarifa kutoka Ulimwengu wa soka Tz zinasema kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone anawapa presha mabosi wa klabu hiyo kuhakikisha kwamba  Antoine Griezmann haondoki klabuni, kwa mujibu wa taarifa kutoka Mundo Deportivo.

Taarifa zilizotoka wiki iliyopita kutoka Hispania zimedai kwamba Barcelona wanatarajiwa kutoa ofa ya Euro Milioni 100 kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwishoni mwa msimu huu.

Griezmann ni mchezaji mkubwa ndani ya Atletico na Simeone anawataka mabosi wa klabu kufanya mazungumzo ya mkataba mpya ili kumzuia kuondoka na kutua timu nyingine msimu ujao.

Comments

Popular posts from this blog