VIPORO VYA SIMBA SASA NI WAZI TAREHE KAMILI HIZI HAPA

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Njombe Mji na Simba SC uliokuwa umeahirishwa, sasa umepangwa kufanyika tarehe 3, Aprili mwaka huu, katika dimba la Sabasaba mjini Njombe.

Awali kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Machi 11 mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuipa Simba nafasi ya kufanya maandalizi ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Al Masry katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Taarifa kutoka ndani ya Bodi ya Ligi zimethibitisha tarehe hiyo, na kueleza kuwa tayari timu zote mbili zimekwishapata taarifa kwaajili ya maandalizi.

Aidha 8 April 2018 kikosi cha Simba kitashuka tena uwanjani dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Comments

Popular posts from this blog

Njia sahihi za kuachana na unywaji wa pombe