SIMBA WAZUNGUMZIA MAENDELO YA JONAS MKUDE
Kiungo mkabaji wa Simba Sc, Jonas Mkude ambaye juzi aliumia mazoezini na kuibua hofu kwa wanamsimbazi, anatarajiwa kurejea mazoezini kesho.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema baada ya kufanyiwa vipimo, imebainika kuwa Mkude alipata majeraha ya michubuko ya kawaida.
Amesema hakuna wasiwasi juu ya afya yake na atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachotarajiwa kusafiri kwenda mkoani Njombe kuivaa Njombe Mji April 03.
Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi hapo jana kwenye uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo.
Wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa wanatarajiwa kujiunga na wenzao muda wowote baada ya kukamilika kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Tanzania dhidi ya DR Congo.
Katika mchezo huo Tanzania ilifanikiwa kuibika na ushindi wa magoli 2-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa, huku Shiza Kichuya akin'gara katika mchezo huo kwa kufunga bao moja na kutengeneza jingine lililofungwa na Nahodha Mbwana Ally Samatta.

Comments
Post a Comment