JUA KWANINI NIYONZIMA ASEMAYANGA HAIMTISHI WALA HAIMPI HOFU NA KUIPONGEZA SIMBA

Na Joseph michael
Haruna niyonzima mchezaji wa SIMBA lakini kabla ya hapo alikuwa akiichezea timu pinzani ya SIMBA yani YANGA ambako mwanzoni mwa msimu huu wa 2017/2018 Niyonzima alihamia SIMBA.Pamoja na kuanza msimu kwa kiwango kisicho ridhisha akiwa SIMBA Haruna Niyonzima pia alikuwa nnje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia.

Lakini habari njeema kwa mashabiki na wapenzi wa SIMBA ni kwamba Niyonzima amerudi uwanjani na ameanza kufanya mazoezi na timu na pia si ajabu tukashuhudia akiecheza mechi ya SIMBA NA NJOMBE MJI ambayo itachezewa mjini njombe.

Baaada ya kufanya mahojiano na CLOUDS FM jana Niyozima alizungumzia mambo mengi sana pamoja na kuelezea hali yake ya kiafya kuimarika vizuri na kuwa teyari kuingia uwanjani japo kuwa alikumbusha kwamba kuhusu maelekezo au nafasi ya kucheza bahado yanategemea sana namna ambavyo mwalimu atapanga mipango yake na daktari wa timu atakavyo elekeza au shauri.Na pia hakusita kuipongeza timu yake ya SIMBA kwa kufanya vizuri kwenye ligi huku akiwambia mashabiki wakumbuke ya kwamba SIMBA haijapoteza hata mchezo mmoja paka sasa kwahiyo hiyo inawapa nafasi kumbwa ya kujiamini kuweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu vodacom Tanzania bara.

Sehemu ambayo mwandishi alimuuliza Niyonzima swali ambalo kidogo lingeweza kuwa gumu kwa Nyonzima ni pale alipo ulinzwa unachukuliaje YANGA kuwafikia kwa pointi ili hali mlikuwa mmemuacha nyuma kwa pointi nyingi hauoni kuwa mnaweza kuukosa ubingwa.Niyonzima alijibu akisema yeye YANGA hai mtishi na wala hai mpi hofu kwa sababu toka ligi imeanza simba imekuwa na kiwango kizuri na pia kwa mechi zilizo baki wachezaji na mwalimu wamejipnga vizuri sana ili kuhakikisha wanachukua point zote thelasini zilizo baki.

Lakini alimalizia huku akisema mashabiki watambue hajafurahia kuwa nnje ya uwanja kwa muda wote huo.Na akamalizia kwa kusema nawashukuru mashabiki SIMBA  kwa kunipokea vizuri na kuweza kunivumilia kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nnje ya uwanja

Comments

Popular posts from this blog