CECAFA yaahirisha tena mashindano ya Undwa 17
Na Joseph michael
Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa mara nyingine tena imeyasogeza mbele mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 inayotarajiwa kufanyika nchini Burundi.
Taarifa za ndani kutoka CECAFA na Shirikisho la Soka nchini Burundi (FFB) ni kuwa mashindano hayo ambayo yalipangwa kuanza April Mosi hadi April 15 sasa yatafanyika kuanzia Aprili 15 Mwaka huu.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana lakini yalisogezwa mbele hadi Mwezi wa nne mwaka na sasa umesogezwa tena mbele ili kupisha mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.
Tayari FFB imethibitisha viwanja vitatu vya Ngozi uliopo katika Mji wa Ngozi, Muyinga na Gitega vyote vilivyopo mjini Bujumbura kutumika katika michuano hiyo.
Maandalizi ya Tanzania
Vikosi vya timu za Tanzania Bara na Zanzibar chini ya umri huo vipo katika maandalizi kwa takribani majuma matatu sasa kujiandaa na michuano hiyo ambayo inaangaliwa kwa jicho la tatu na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Aidha nchi 10 ambazo ni mwenyeji Burundi, Uganda, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Ethiopia, Tanzania Bara, Somalia, Djibouti, Zanzibar na Rwanda zikitarajiwa kushiriki michuano.
Na hii ni mara ya tatu kwa mashindano hayo kufanyika, Mara ya kwanza yalifanyika nchini Burundi mwaka 2007 na Burundi kutawazwa mabingwa huku mwaka wa pili yakifanyika Kenya mwaka 2009 ambapo Uganda walinyakua ubingwa

Comments
Post a Comment