MANCHESTER CITY HAIKAMATIKI YAINYOA EVERTON

Na Yego Sholla


Full Time: EPL

Magoli matatu ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Leroy Sane, Gabriel Jesus na Raheem Sterling yametosha kuipa pointi tatu muhimu kabisa Mancheste City kuelekea ubingwa wa EPL.

Kevin De Bruyne ametengeneza goli moja na hivyo kufikisha ' assists ' 15 , tano pungufu ya rekodi ya Thierry Henry ambaye alifikisha ' assists ' 20 .

Man City sasa wanahitaji ushindi wa mechi ijayo dhidi ya Man United tarehe 7 dimba la Etihad kuwa mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2017/2018 .

Ederson ameruhusu goli moja hivyo anabakiwa na idadi ile ile ya ' Clean Sheets ' 14 mbili pungufu ya kinara David De Gea mwenye 16.

Comments

Popular posts from this blog