Hatua sita muhimu za matibabu ya Kigimbi


Na Joseph michael

Wanasoka hawa wakulipwa walisaidia Tanzania, Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
SI kipofu kaona mwezi, bali ni uwezo binafsi na kubadilika kiwango, hayo yalionekana dhahiri kuwepo kwa mafaniko kwa wanasoka wetu wanaocheza nje ya nchi Mbwana Samatta na Simon Msuva.

Wanasoka hawa wakulipwa walisaidia Tanzania, Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ni kawaida kwa wanasoka hawa kipindi kama hiki huwa wanashiriki ligi wanazocheza pamoja na mechi zakimataifa, ushiriki huu unawaweka katika hatari ya majeraha pamoja na uchovu wa mwili.

Kwa wanasoka, misuli ya kigimbi inamuwezesha kufanya mambo mengi ikiwamo kupiga mpira na ni eneo mojawapo linalopatwa na majeraha ikiwamo kuchanika misuli yake.

Wiki hii ilikuwa wiki ya michezo ya kirafiki ya nchi moja na nyingine, lengo ni kujiandaa na kinyang’anyiro cha Kombe la Dunia kule Russian 2018 na wengine kupandisha viwango vya Fifa.

Wanasoka wanaocheza ligi za kulipwa kama akina Samatta na Msuva huwa na majukumu mazito.

Wanapopata majeraha ya michezo, hupewa mpangilio maalumu wa matibabu wenye lengo la kuwawezesha kupona na kurejea uwanjani wakiwa imara na wenye stamina.

Majeraha ya kigimbi au kiazi cha mguu ni kati ya majeraha yanayowasumbua wana soka wengi duniani. Leo tutaona hatua sita zinavyofanyika kumtibu mwenye jeraha la kigimbi au kiazi cha mguu.

Awamu ya kwanza; kupunguza maumivu na shambulizi la mjibizo wa mwili pale unapokuwa na majeraha ya kigimbi. Zipo hatua za awali na zinazochukuliwa haraka ili kuulinda mguu uliojeruhiwa usiendelee kupata majeraha.

Mchezaji hupumzishwa, kuwekewa barafu, jeraha la kigimbi hukandamizwa kutumia bendegi yenye kuvutika kama mpira na unyanyuaji mguu kuzidi kifua.

Pamoja na haya yote, dawa za maumivu za kupaka au kupulizia pia zinatumika kuzuia maumivu zaidi.Kundi la misuli ya kigimbi ni misuli yenye nguvu inayoweza kutoa msukumo mkubwa wa kuweza kukimbia, kuruka na kutembea.

Katika hatua za mwanzoni mtu aliyejeruhiwa anaweza kutembea kwa kuchechemea, hivyo kupumzishwa husaidia kuzuia shinikizo la uzito wa mwili katika miguu na kuepusha madhara zaidi.

Uvikaji wa vifaa tiba maalumu kama kiatu maalumu, usaidizi wa kutembea na kiti au magongo maalumu ya kutembelea ni moja ya tiba muhimu sana.

Kufanya hivi kunasaidia mguu kupata utulivu na kuwa mahali pamoja bila kucheza cheza, vilevile husaidia kutokuwapo au kupunguza kwa shinikizo la uzito wa mwili hivyo kupunguza kujijeruhi zaidi.

Barafu ni moja ya nyenzo muhimu katika matibabu ya awali ili kupunguza maumivu na uvimbe.

Inaweza kuwekwa kwa dakika 10-20 kwa kila masaa 2-4, weka pale unapohisi mguu umepata moto au una vuguvugu.

Ingawa dawa za maumivu zinaweza kutumiwa kukata maumivu na uvimbe mara nyingi huepushwa katika saa 48-72 za mwanzoni kwani dawa hizi zinaweza kuchangia damu kuongezeka kuvuja katika jeraha.

Katika saa za awali kabisa utakuta baadhi hupewa paracetamol ya vidonge tu kwani ndio hufanya kuwa salama na kuvuilika na mwili wa aliyejeruhiwa pasipo tatizo lolote.

Kadiri unavyoimarisha ukandamizaji kwa kutumia clip bandage husaidia kuupa nafuu tishu laini zilizo jeruhiwa na pia kuzuia damu kujivujisha ndani ya mguu.

Kuuweka mguu uliojeruhiwa juu kidogo kuzidi kifua chako ukiwa umelala au kukaa husaidia kurudisha damu kutoka eneo la mguu kwa haraka, hivyo kupunguza uvimbe kwa haraka.

Awamu ya tatu: Kurudishia mijongea kama ilivyokuwa awali

Kama zoezi la kwanza litaenda vizuri kama inavyotakiwa ubora na ufanisi wa misuli hiyo huweza kurudi kama ilivyokuwa awali.

Ukarabati wa jeraha na kujiunga huchukua takribani wiki sita tu.

Wakati huu dhumuni linakuwa ni kusaidia kuzuia gamba la jeraha lilojiunda liwe imara na ufanisi mzuri ili kusiwepo na kujirudia kwa majeraha haya hapo baadaye.

Ni muhimu sana kuliimarisha na kulirudishia ufanisi jeraha lilounga kwa kutumia kusingwa (massage), kuinyoosha misuli hiyo na kuimarisha mishipa ya fahamu na damu kwa mazoezi mepesi ya viungo.

Dalili na viashiria kuwa sasa jeraha limepona ni pamoja kuweza kutembea bila kuchechemea na kuweza kufanya ile mijongeo mbalimbali na kuinyoosha misuli ya kigimbi pasipo kikwazo.

Awamu ya nne: kuurudishia kigimbi uwezo wa kunyanyua mwili

Ukakamavu na nguvu za misuli hii ni lazima uimarishwe taratibu kwa kuondakana na ile hali yakutokuweka shinikizo la uzito na kuanza kuweka shinikizo la uzito wa mwili kidogo kidogo mpaka hapo baadaye kuweka shinikizo kubwa la uzito.

Hii ina maana kama majeruhi alikuwa anatumia kifaa au alikua hautumii mguu kuukanyagia moja kwa moja sasa anapaswa kuacha na kuanza kutembea bila usaidizi wa chochote.

Baada ya juma moja hadi mawili anawezaa kuanza kutembea, kisha akaanza kujinyanyua kidogo kidogo na kuuvuta mwili na kukimbia kidogo kidogo na baadaye akaanza kuruka ruka.

Kuruka na kukimbia kwa nguvu zaidi inamaana kuwa sasa eneo hilo la kigimbi linapata shinikizo la uzito wa mwili na hapo ndipo wataalamu wa viungo hujiridhisha kuwa eneo limepona na mchezaji huendelea na programu ya mazoezi ya viungo na mafunzo.

Awamu ya tano: kurudishia kigimbi uwezo wa kudhibiti kudondoka na kuukalisha mwili chini.

Misuli ya miguu ndio inayosababisha kufanya mielekeo miwili muhimu, yaani kukunyanyua na kukudhibiti kudondoka/kukuvuta chini.

Hatari ya kujitonesha kwa misuli na kuchanika tena hutokea wakati wa unyooshaji misuli.

Kuepusha jambo hili mtaalamu wa viungo hutoa mwongozo wakati wa program maalumu ya mazoezi ya viungo yanayomwezesha kuhimili kujivuta chini kama vile kuchuchuma, kupiga msamba, kukaa na kuruka kichura haya yanafanyika tu endapo hali ya jeraha itaruhusu.

Awamu ya sita: Kurudisha uwezo wa kukimbia kasi, ukakamavu na kuongeza umakini na ufanisi.

Majeraha ya kigimbi hujitokeza sana pale kunapokuwa na shughuli zinazohitaji kukimbia kasi, hali hii huleta msukumo mkubwa mwilini hasa kujikunja na kujikunjia kwa misuli.

Ili kuzuia kujirudia kwa majeraha unapokuwa unarudi katika mchezo, mtaalamu wa viungo atakupa mwongozo maalumu wa mazoezi unaokuelekeza mambo muhimu katika programu ya mazoezi ili kukujengea uwezo wako kama livyokuwa awali. Ingawa pia itategemea na mchezo upi unaocheza na nafasi ipi na kasi unayohitajika kuwa nayo, utapewa tu mazoezi maalumu.

Comments

Popular posts from this blog