Azam Tv yamwaga noti Kombe la KAGAME
By Joseph michael
FRIDAY MARCH 30 2018
Nairobi, Kenya. Katika kuhakikisha mashindano ya Kombe la Kagame yanafanyika Dar es Salaam mwaka huu Azam TV imedhamini mashindano hayo kwa kiasi cha Kshs40 milioni (sawa Tsh80 milioni).
Katibu mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika mashariki na kati (Cecafa) Nicholas Musonye amesema amepokea Kshs200 milioni kuhakikisha michuano ya baraza hilo ya kila mwaka inafanyika bila kukosa.
Kombe la Kagame litaandaliwa Tanzania Juni huku lile la Chalenji litafanyika nchini Kenya mwezi Novemba. Mashindano hayo mawili inafadhiliwa na Azam TV ya Tanzania kwa kitita cha Kshs40 milioni.
Azam Fc ni mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame watashiriki kulitetea taji lao wakati Yanga ni mabingwa wa Tanzania na kuna uwezekano wa Simba kupewa nafasi ya kushiriki michezo hiyo
Mbali ya mashindano hayo Musonye pia alizungumzia mashindano ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 inayotarajiwa kuchezwa Burundi Aprili 14 hadi 29 na yale ya vijana chini ya miaka 20, yatafanyika Uganda Septemba.
Pia, kuna mashindano ya wanawake yatafanyika nchini Rwanda mwezi Mei na ya ufukweni yatakayofanyika Uganda vile vile mwezi wa Mei.
“Hizi fedha Sh 200 milioni zitatumika katika mashindano manne ya U17 kwa wanaume pamoja na yale ya wasichanaU17, na soka la Ufukweni ambapo Kshs50 milioni zimetengwa kila mashindano,” alisema Musonye.
“Mechi za U17 zinaanza katikati ya mwezi ujao ili kufaidi timu katika maandalizi ya kufuzu AFCON ya hao chipukizi itakayoandaliwa nchini Tanzania mwaka ujao,” aliongeza.
Hii ni afueni kwa wapenzi wa soka kanda hii baada ya kukosa mfano mashindano ya U17 kwa miaka tisa huku ya wanawake mwisho yalifanyika mwaka 2016 kwa sababu ya kukosa fedha.
Burundi, Kenya, Uganda, Somalia, Djibouti, Eritrea, South Sudan, Sudan, Tanzania, Zanzibar, Ethiopia na Rwanda wote wanatarajiwa kushiriki katika mechi zitakazoandaliwa miji mitatu tofauti ya Ngozi, Muyinga na Gitega kule Burundi.
Comments
Post a Comment