MAKALA: WANAUME WACHACHE KATIKA WENGI KISOKA

NA GHARIB MZINGA

Katika soka duniani, kuna makundi mawili ya watu wale ambao wameweza kufanikiwa vilivyo kupitia soka. na wale ambao hawakufanikiwa sana. Kufanikiwa kisoka si kuapata pesa nyingi tu lah hasha!!! bali hata kuweka rekodi na kumbukumbu kwa mdau na mchezaji ambazo zitamfanya watu wamzungumzie vizuri kila linapotajwa jambo lake.

Kuna wachezaji wengi sana wamecheza soka katika nchi hii tangu ikiwa Tanganyika mpaka sasa Tanzania. Huenda miaka mingi ya 1930 mpaka 1990 maendeleo ya sayansi na teknolojia yalizuia watu kuona soka la ndani kwa ufasaha. lakini bado kuna rekodi kubwa zimewekwa na baadhi ya wanaume wa shoka mpaka leo zinaishi, pia kuna wachezaji wa kizazi kipya nao wameweka zakwao ambazo zitaendelea kukumbukwa muda wote mpaka atokee mwengine kuzivunja.

Mohamed hussein daima "mmachinga" huyu ni mchezaji wa zamani wa yanga na simba sc anashikiria rekodi ya kua mfungaji bora wa muda wote mwenye goli nyingi katika msimu mmoja. alifunga goli 26 mwaka 1999.

Nadir Haroub canavaro. Huyu ni beki mkongwe kisiki wa Club ya Dar es salaam Young africa. alijiunga na club hiyo mwaka 2006. ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kubeba mataji mengi ya ligi kuu tTanzania bara. mataji 8.

Abdala Kibaden Mputa, huyu ni mchezaji nguli wa zamani wa simba sc, anashikiria rekodi ya kua mchezaji pekee aliyefunga Hat trick katika pambano kubwa africa simba dhidi ya yanga. Alifanya hivyo mwaka 1977 katika ushindi wa goli 6-0.

Joel Bendera, Huyu alikua mchezaji, lakini mafanikio makubwa aliyapata akiwa mwalimu  (kocha) ndiye mtanzania aliyeipeleka Taifa stars Lagos (nigeria) katika fainali za Afcon mwaka 1980.

Sunday Manara, Huyu ni mchezaji wa zamani wa Yanga, sifa yake kubwa ilikua ni uwezo wa hali ya juu wa kusakata kabumbu kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii. alibatizwa jina la computer.

Mrisho Khalfan Ngassa, huyu anakipiga club ya ndanda kwa sasa ni mchezaji wa zamani wa pamba, kagera, yanga, azam, simba n.k anashikilia rekodi ya mchezaji mwenye goli nyingi katika timu ya taifa. (taifa stars) goli 21.

Peter Augustino (Tino). Mstaafu huyu alipata mafanikio akichezea club ya Pan africa miaka ya 1980.  rekodi yake kubwa ni Kufunga goli la uwezo mjini ndola dhidi ya zambia, katika mchezo wa marudiano wa kufuzu kucheza afcon nigeria. goli ambalo liliipatia taifa stars ticket ya kushiriki Afcon mwaka 1980.

Licha ya rekodi hizo murua, kuna walinda milango ambao wamefanya makubwa katika soka la tanzania na kubakia wakizungumzwa kila uchao. Stephan Nemes (masajage) amechezea Taifa stars miaka 15 mfululizo, Mohamed Mwameja sifa yake kuu ni kuchomoa mikwaju ya penalt. Juma pondamali Mensah, Iddi Pazi, na Othman Mambosasa.

MWISHO. makala hii ingependa kukipongeza kikosi cha Tukuyu stars banyambala kilichopanda daraja na kuchukua ubingwa wa ligi daraja la kwanza (sasa ligi kuu) mwaka 1986 kisha ikashuka daraja.

baadhi yao ni Mbwana Makata, Betwell Africa, Sekilojo Chambua, Daniel Chundu, Asanga Aswile, Kelvin Haule, na Chachala Muya.

Comments

Popular posts from this blog