SERGEJI MILINKOVIC - SAVIC ANATHAMANI YA MIL 78

Na Yego Sholla

Mkurugenzi wa Lazio, Igli Tare amesema kiungo wao  Sergej Milinkovic-Savic  ana thamani ya Pauni Milioni 78.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Serbia amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kutua vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya vikiwemo Juventus, Real Madrid, Barcelona, Paris Saint-Germain, Liverpool na Manchester United .

" Sijui ni thamani  gani anaweza kuwa nayo na sitaki hata kuanza kufikiria . Lakini ni kiasi zaidi ya Pauni milioni 70 mpaka Pauni Milioni 78. Sergej ni muhimu sana kwetu na bado hata hajafikia daraja la kipaji chake halisi."

" Siku zote kuna wachezaji wengi ambao unaweza kuwatafuta na kuwaboresha . Nataka kuwa wazi kuhusu hili, Lazio hawajawahi kuweka ada au kuwahi kuulizwa chochote kuhusu Milinkovic. Tulipokea ofa msimu uliopita lakini hatukuzifanyia kazi."

Comments

Popular posts from this blog