LOUIS VAN GAAL WAMALIZA TOFAUTI ZAO NA KOCHA WA MANCHESTER UNITED JOSE MOURINHO
Na Yego Sholla
Louis van Gaal ameonekana kutengeneza amani na kocha wa Manchester United Jose Mourinho huku akimkosoa Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward.
Mdachi huyo aliitumikia United kwa misimu miwili lakini alifukuzwa kazi katika siku ambayo walitwaa taji la FA mwaka 2016 na mwaka jana alisema kwamba kuondoka kwake ndani ya United na kuajiriwa kwa United " Halikuwa jambo la busara "
Van Gaal alikutana na Mourinho ndani ya Anfield mapema msimu huu ambapo United walitoka sare dhidi ya Liverpool na alidai kwamba Mreno huyo huwa mara nyingi anashindwa kujidhibiti lakini sasa hivi anaelewa kwamba kila kocha ataitaka kazi ya Manchester United.
" Sina tatizo na Manchester United, kila kocha anataka kuinoa United, ni moja ya klabu kubwa Duniani ." Ameliambia jarida la Bild.
" Nafikiri hata Jose alikuwa anaitaka hiyo kazi pia , licha ya kwamba aliweza kuipata kazi hiyo akimaliza nafasi ya 13 , alikuwa na nafasi katika timu nzuri ya Chelsea, nilikuwa nafasi ya nne. Bado simlaumu ."
" Kitu ambacho nakiona sio sahihi ni pale Mtendaji Mkuu anaposema, tuna furaha kabisa na wewe , usiamini vyombo vya habari. Halafu unatwaa taji la FA na baaade unafukuzwa."
Van Gaal pia anaamini kwamba Pep Guardiola, ambaye aliwahi kutwaa nae mataji mawili ya La Liga akiwa Barcelona kwa sasa ndio kocha bora katika Ligi na kusema kwamba angependa kuibadilisha United kucheza soka kama lile la City.
" Pep Guardiola kwangu mimi , kwa sasa ndio kocha bora wa Ligi kuu ya Uingereza. Pep ameifanya Man City kuwa mashine."
" Anaonyesha aina ya soka ambalo ningependa Manchester United yangu kucheza hivyo. Lakini ana wachezaji wazuri wa kucheza hivyo. Kwangu mimi huo mchanganuo ungechukua muda mrefu . Kwa bahati mbaya , sikupata muda."

Comments
Post a Comment