MAGULI KAZUNGUMZA KUHUSU KURUDI UWANJANI BAADA YA KUKAA NJE MIEZI 6

Na joseph michael
March 30, 2018  MICHEZO

Mshambuliaji wa zamani wa Ruvu Shooting, Simba, Stand United za ligi kuu tanzania bara na Dhofar ya Oman Elias Maguli baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi sita bila kucheza, hivi karibuni atatangaza timu atakayocheza msimu ujao.

Maguli ambaye walishindwa kufikia mwafaka na Polokwane City ya Afrika kusini iliyokuwa ikitaka kumsajili kipindi cha dirisha dogo alichelewa usajili wa tanzania hivyo kulazimika kukaa nje kwa kukosa timu.

Mshambuliaji huyo amesema siku si nyingi atatangaza timu atakayocheza msimu ujao, inawezekana ikawa ya VPL au nje ya nchi.

“Sasa hivi watu wanapambana kuzinusuru timu zao zisishuke daraja wengine wanataka ubingwa kwa hiyo wapo makini sana na ligi kumalizia mechi zilizobaki, watakapomaliza michakato ya usajili itaanza kwa hiyo nitajua ni hapa nyumbani au nje.”

“Msimu ujao au hivi karibuni naweza nikaweka wazi ni wapi nitaelekea kwa sababu ndani ya miezi sita nimekaa bila kucheza.”

Comments

Popular posts from this blog