Alliance Queens mambo safi matokeo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara
Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara upande wa wanawake hatua ya nane bora kati ya Alliance Queens na Kigoma Sisterz umemalizika kwa vurugu baada ya benchi la ufundi la wageni kumlaumu mwamuzi wa mchezo huo kutotenda haki. Mtanange huo ambao ulikuwa mkali na wakusisimua umefanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kushuhudia Alliance wakiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0. Bao la ushindi la Alliance lilipatikana katika dakika ya 43 kupitia kwa mshambuliaji hatari Janeth Maturanga ambaye aliukuta mpira uliochongwa na Sarah Joely Kaskazini Magharibi mwa lango la Kigoma Sisterz. Mchezo huo ulikuwa na upinzani muda wote ambapo kila timu ilicheza vizuri kwa dakika 45 wakianza Alliance Queens na baadae katika kipindi cha Kigoma Sisterz kuonekana kutawala mchezo. Kuibuka kwa vurugu Mara baada ya mchezo kumalizika wachezaji na benchi zima la ufundi la Kigoma Sisterz liliwarukiwa waamuzi wakiwalaumu kuwapendelea Alliance ambapo katika purukushani hizo kipa wa Kigoma Mw...