Masikini Real Madrid kulikoni

Hakika kisicho riziki hakiliki, Real Madrid wakiwa wamepanda mbele wakiongozwa na nahodha wao, Sergio Ramos , Espanyol wakatoka nyuma kwa 'Counter Attack ' ya kasi na kufunga goli dakika ya 93 na kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Madrid Ulimwengu wa soka Tz umeripoti kuwa

Kwa matokeo hayo Real Madrid wanadondosha pointi zote tatu badala ya mbili na kubaki nafasi ya 3 , wakikwa wamecheza mechi 26 pointi 51 , huku nafasi ya nne Valencia ana pointi 49 pointi mbili pungufu ya Madrid wakiwa wamecheza mech 25 kwahiyo ana nafasi ya kumtoa Real katika nafasi ya tatu.

Barcelona na Atletico Madrid wamepata upenyo mkubwa wa kuongeza wigo dhidi ya Real, lakini wikiendi hii wanacheza wao kwa wao ( Barcelona Vs Atletico Madrid ) Nou Camp.

Comments

Popular posts from this blog