Alliance Queens mambo safi matokeo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara
Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara upande wa wanawake hatua ya nane bora kati ya Alliance Queens na Kigoma Sisterz umemalizika kwa vurugu baada ya benchi la ufundi la wageni kumlaumu mwamuzi wa mchezo huo kutotenda haki.
Mtanange huo ambao ulikuwa mkali na wakusisimua umefanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kushuhudia Alliance wakiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Bao la ushindi la Alliance lilipatikana katika dakika ya 43 kupitia kwa mshambuliaji hatari Janeth Maturanga ambaye aliukuta mpira uliochongwa na Sarah Joely Kaskazini Magharibi mwa lango la Kigoma Sisterz.
Mchezo huo ulikuwa na upinzani muda wote ambapo kila timu ilicheza vizuri kwa dakika 45 wakianza Alliance Queens na baadae katika kipindi cha Kigoma Sisterz kuonekana kutawala mchezo.
Kuibuka kwa vurugu
Mara baada ya mchezo kumalizika wachezaji na benchi zima la ufundi la Kigoma Sisterz liliwarukiwa waamuzi wakiwalaumu kuwapendelea Alliance ambapo katika purukushani hizo kipa wa Kigoma Mwasiti Juma alimchapa kibao mwamuzi na kulimwa kadi nyekundu.
Aidha kama si juhudi za wachezaji wa Kigoma Sisterz kumzuia mwalimu wao Daudi Lawrence basi mambo yangekuwa mabaya zaidi kwani kocha huyo alionekana mwenye hasira ya mbogo lakini baadae alitulia.
Matokeo hayo yanawafanya Alliance Queens kufikisha alama 3 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 4-0 huku Kigoma Sisterz wao wakisaliwa na alama 3 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Simba Queens.
Matokeo mengine:
FT: Evergreen Queens 0-8 JKT Queens
FT: Baobab Queens 1-1 Panama Girls

Comments
Post a Comment