YANGA VS TOWNSHIP ROLLERS KUCHEZESHWA NA WARUNDI LIGI YA MABINGWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6-2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 16.30 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

Mechi ya marudiano itachezwa Machi 17-2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.

Comments

Popular posts from this blog