KABLA YA YANGA KUIVAA NDANDA HILI NI OMBI LA JERRY MURO KWA WACHEZAJI NA MSHABIKI WA YANGA

Aliyekuwa Afisa Habari wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, amewataka mashabiki na wanachama wa kufanya maombi na dua ili timu hiyo iweze kushinda leo.

Yanga itashuka dimbami leo February 28 katika kukamilisha raundi ya 19 dhidi ya Ndanda mchezo huo ukitarajiwa kupigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kuanzia saa 16:00 jioni

Jerry Muro ameeleza kuwa Yanga haiko vizuri kichumi hivi sasa tofauti na msimu uliopita, hivyo ameomba sala na dua za wanachama zifanyike ili kuisadia timu hiyo huku akisema ligi ya msimu huu ni ngumu.

Sanjari na hayo, Muro amewaomba wachezaji wa Yanga waweke fadhila mbele kuliko maslahi, wakumbuke kipi Yanga imewafanyia, na si kuendekeza pesa kwani watakuwa wanaiharibia timu malengo.

Muro ameeleza ni wakati sasa ufikie kwa wachezaji wa timu kujituma zaidi kama ambavyo Simba walikuwa wakifanya kipindi kile hali ya uchumi kwao haikuwa nzuri kama ambavyo Yanga walivyo sasa.
"Wachezaji wanatakiwa watambua hali ya kifedha ilivyo klabuni, wanapaswa wajitume zaidi Uwanjani na si kuendekeza masilahi, vema wakakumbuka Yanga imewafanyia mangapi mazuri kuliko kujikita zaidi kwenye fedha".
Muro amesisitiza zaidi kwa kusema Yanga sasa inahitaji zaidi nguvu na sapoti ya mashabiki, sambamba pia kuwepo na maombi ili timu iweze kufanya vizuri.

Comments

Popular posts from this blog