MATOKEO NA MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA FEBRUARY 28-2018
Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo Jumatano ya February 28-2018 kwa mchezo mmoja uliokuwa unakamilisha raundi ya 19 kati ya Ndanda Fc ya Mtwara dhidi ya Young Africans ya Dar es salaam.
Mchezo huo ulianza majira ya saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Nangwanda-Mtwara, ambapo Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Pius Charles Buswita katika dakika ya 06 na Hassan Ramadhan Kessy dakika ya 29.
Bao pekee la Ndanda limefungwa na Nassor Kapama sekunde chache tu kipindi cha pili kilipoanza akiunganisha krosi ya mshambuliaji wa Zamani wa Yanga na Simba Mrisho Khalfan Ngassa.
Kwa matokeo hayo Yanga inajikusanyia alama 40 katika michezo 19 pointi 5 nyuma ya Vinara Simba wenye alama 45 kwenye michezo 19 pia.
Huu ni msimamo wa ligi kuu baada ya kukamilika kwa raundi ya 19 ukionesha Yanga ikizidi kuifukuzia Simba kileleni huku tofauti ikiwa ni pointi tano pekee, wakati Ndanda FC ikiendelea kubaki katika nafasi yake ya 13.

Comments
Post a Comment