Fahamu kilicho sababisha Joseph kanakamfumu kufungiwa na tff

SAKATA LA KANAKAMFUMU NA MVUVUMWA.

KAMATI YA MAADILI
Kamati ya maadili ya TFF iliyokutana tarehe 3 na 17 feb ilipitia na kutoa hukumu za kutoa taarifa za kugushi katika leseni za usajili za wachezaji..watuhumiwa walifikshwa mbele ya kamati hiyo...tuhuma ni kutokana na mechi namba 26 kundi A fdl iliyofanyika october 29 mwaka 2017 kati ya Mvuvumwa na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo iliwachezesha wachezaji watano ambao ni Elias Costa Eliasi jz no 5, Lukwesa Joseph Kanakamfumu jz no 7, Dunia Abdallah Dunia jz no 1, Dotto Justin Kana jz no 12 na Mwarami Abdallah Mwarami jz 8.

Walioitwa kwenye kamati ni hao wachezaji lakini pia viongozi Yared Fubusa (Mwenyekiti na Mmiliki wa timu), Ramadhani Kimilomolilo (Katibu wa timu ya Mvuvumwa) pamoja na Joseph Kanakamfumu (Kocha na mratibu wa timu) Yusuph Makoya (mratibu wa zamani)

Makosa yao
1. Kutoa taarifa zisizo sahihi....kuhusu usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41.. kifungo kidogo cha 12 cha kanuni za fdl tolea la 2017..

2. Kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73 kifungu kidogo cha 7 kanuni za maadili.

Kwa upande wa wachezaji kosa lao ni kucheza mchezo husika huku wakijua usajili haujakamilika.

HUKUMU
Wachezaji wao wameachiwa kwa kuwa hawakuhusika katika udanganyifu huo..

Kocha Joseph Kanakamfumu.... yeye amekutwa na makosa yote mawili..kutoa taarifa zisizo rasmi na udanganyifu ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41 kifungu kidogo cha 12 ya kanuni ya fdl na kughushi leseni...
KAMATI IMEMFUNGIA KUTOJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA MPIRA KWA MIAKA 5, na adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73 kifungu kidogo cha 7 cha kanuni za maadili toleo la 2013.  Ramadhani Kimilomilo amekutwa na hatia ya kughushi leseni ... na yeye pia amefungiwa kwa kipindi cha miaka 5 ..... Mwenyekiti na Mmiliki wa Mvuvumwa fc ... kamati imemtia hatiani kwa kosa hilohilo .... alipoitwa ajitete na kamati alisema tff ni wapumbafu sababu yeye ni muhanga wa tukio hilo.. kamati imempa adhabu zifuatazo
1. Kwa kutoitikia wito wa kamati anafungiwa mwaka 1 pamoja na faini ya sh 3m.
2. Kosa la kughushi ... amefungiwa kwa miaka 5.

Adhabu kwa mujibu ya kifungu 73 kifungu kidogo 3.
Adhabu zinakwenda kwa pamoja.

Comments

Popular posts from this blog