MANARA ATAJA COMBINATION BORA KUWAHI KUTOKEA KWENYE VPL KTK KIPINDI CHA MIAKA 10 ILIYOPITA.

Ligi kuu Tanzania Bara imefikia raundi ya 20 sasa baada ya raundi 19 kukamilika leo February 28-2018 kwa mchezo mmoja uliozikutasha timu za Ndanda vs Yanga.

Katika michezo hiyo 19 klabu ya Simba imefanikiwa kuvuna alama 45 na mabao 38.
Okwi ndiye kinara wa mabao ligi kuu Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 16 huku John Bocco akiwa nafasi ya tatu na mabao yake 10, Shiza Kichuya aliyebadilishiwa majukumu na benchi jipya la ufundi, ana mabao 7.

Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Sunday Manara, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ametaja combination bora kuwahi kutokea kwenye VPL katika kipindi cha miaka kumi 10 iliyopita.

Combination hiyo imebebwa na kiungo Shiza Kichuya na washambuliaji wawili John Bocco na Emanuel Okwi kwa mafanikio waliyoipa Simba mpaka sasa msimu huu na kuibatiza jina la KIBO

Katika ukurasa huo Manara ameandika: Haijaandikwa na kusemwa kokote..najua hujui ngoja nikujuze..,

Okwi, Bocco na Kichuya kwa pamoja wamefunga magoli 38 kati ya magoli 52 ya Simba kwenye michezo 22 ya mashindano rasmi waliyocheza Simba hadi sasa.

Mashindano rasmi waliyocheza ni pamoja na Ligi kuu,kombe la Shirikisho CAF na Kombe la Shirikisho la Azam.

Ukiachana na magoli hayo ambayo ni sawa na 73%ya magoli yote ya Simba 52, wachezaji hao kwa pamoja wameassist magoli 33.

Ndio combination bora kuwahi kutokea kwenye VPL ktk kipindi cha miaka kumi nyuma..iite KIBO..Kichuya.Boko na Okwi.....rudia tena KIBO

Comments

Popular posts from this blog