Courtois ashangazwa na maamuzi ya Conte.
Thibaut Courtois amehoji maamuzi ya kocha wake wa Chelsea Antonio Conte kumtoa uwanjani Eden Hazard katika mechi ya kichapo cha 2-1 dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili.
Chelsea wametoka kwenye timu nne za juu baada ya magoli kutoka kwa Romelu Lukaku na Jesse Lingard kuipa United ushindi baada ya Chelsea kutangulia kupitia goli la Willian.
Goli la ushindi la Lingard lilikuja dakika mbili baada ya Hazard kutolewa na Conte huku Pedro akichukua nafasi ya Mbeligiji huyo.
Baada ya hapo Chelsea waliachwa uwanjani bila ya mchezaji wao mbunifu wakiwa wanatafuta kurejea mchezoni na Courtois ameonyesha kushangazwa kwake kwa kutolewa Mbeligiji mwenzake na kusisitiza kwamba Hazard alitakiwa kucheza kwa dakika 90.
" Sina maelezo kuhusu kutolewa kwa Hazard. Sikutegemea yeye kutolewa lakini ni maamuzi ya kocha."
" Inabidi atoe maelezo. Siwezi kumuangalia kichwani."
" Wachezaji kama Hazard inabidi wachezaji dakika 90 uwanjani. Muda wowote anaweza akaleta kitu zaidi kwenye eneo la ushambuliaji."
Conte yeye alisema kwamba Hazard alishindwa kuhimili daraja lake kipindi cha pili na kutolewa kwake ilikuwa ni uamuzi wa kimbinu .
" Hapana, Hazard hakuumia. Ilikuwa badiliko la kimbinu."
" Lazima uwe na kiwango kile kile kwa dakika 90, hatukuwa na uwiano mzuri. Na kila mchezaji uwanjani lazima afanye sana kazi akiwa na mpira, bila mpira , vinginevyo tunapoteza uwiano."
" Nafikiri alipoteza nguvu sana kwasababu kipindi cha kwanza alikimbia sana. Kipindi cha pili alianza vile vile kama cha kwanza , lakini pindi nikiona mchezaji amechoka , kazi yangu ni kutafuta suluhisho lingine."Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa kijamii wa Ulimwengu wa soka Tz

Comments
Post a Comment