REKODI 2 MPYA ZA NICHOLAS GYAN WA SIMBA

Mshambuliaji wa pembeni wa Simba Sc Nicholas Gyan amefunga goli mechi ya Kirafiki dhidi ya Hard Rock, katika ushindi wa mabao 5-0 kwenye dakika ya 48 akimalizia pasi ya 'Mo' Ibrahim ililikuwa September 03-2017, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru-Dar es salaam.

Gyan amefunga tena juzi dhidi ya wakata Mbao wa Mwanza akimalizia krosi ya Mghana mwenzake Asante Kwasi kwenye ushindi wa mabao 5-0, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam.

Hizi ni kumbukumbu zangu juu ya mechi zote za Simba alizocheza Nicholas Gyan kuwa ana jumla ya goli 2 na sio moja.

Ambapo kwenye ligi ana goli 1 na goli jingine kwenye mechi ya kirafiki.

Hivo Gyan ameweka rekodi mpya ya kufunga kwenye ushindi wa mabao 5-0 au (5G) wenyewe wanauita walioupata Simba Sc msimu huu kwenye michezo yote.

Rekodi ya pili Gyan ameweza kufunga goli lake la kwanza kwenye ligi toka asajiliwe na Simba Sc, majira ya joto akitokea Ebusua Dwarfs inayoshiriki ligi kuu kwao Ghana

Comments

Popular posts from this blog