MCHEZO WA NDANDA VS YANGA UTAKUWA MGUMU, LAKIN HILI NDILO TATIZO LA NDANDA

Kwa kuutazamia mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara maarufu kama Vodacom premier league baina ya wenyeji Ndanda FC dhidi ya Yanga sc

Bila shaka utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa kutokana na nafasi katika msimamo wa ligi lakini pia ubora vikosi na mabenchi ya ufundi kwa timu zote mbili

Ndanda FC wao wapo kunako nafasi ya 13, baada ya kushuka dimbani mara 18, ni wazi hii sio nafasi nzuri kwao itakayofanya wabakie salama mwishoni mwa ligi, hivyo wataingia katika mchezo huu kwa lengo moja tu la kusaka alama tatu muhimu ili kujiondoa katika miongoni mwa timu zilizopo kwenye janga la kutelemka daraja

February 28, 2018 Ndanda FC vs Young Africans SC 4:00 pm Nangwanda

Yanga sc, wao ndio mabingwa watetezi na wapo katika nafasi ya pili, wakiwa na alama 37, baada ya kushuka dimbani mara 18, hivyo huitaji wa alama tatu utakuwa ni mkubwa sana ili kuendelea kujiweka vizuri katika mbio za kutetea taji hilo la ligi kuu

Kimbinu na kiufundi

Ndanda FC inayofundishwa na kocha Malale Hamsini, mara nyingi wamekuwa wakitumia mfumo 4-5-1 ni wazuri kiasi kwenye kumiliki mpira pressing na cutoff

Safu yao ya ulinzi imekuwa na makosa mengi binafsi, man to man densive system ni aina mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia huku tatizo la kufanya pre marking limeonekana kuwasumbua sana, hivyo katika mchezo wa leo watapaswa kuongeza umakini wakati kwenye marking kutokana leo wanacheza na timu yenye watu wengi wenye uwezo wa kufunga

Eneo la kiungo hapa mahala ambapo matatizo mengi ya timu huanzia licha ya kuwa na namba kubwa sana, lakini wamekuwa wakikosa muunganiko mzuri wa kimbinu na mara nyingi wamekuwa wakipoteza mipira kuanzia katikati ya kiwanja pressing, marking yao kwenye high line imekuwa sio nzuri sana, licha ya uwepo wa watu wenye uzoefu mkubwa kama Jabir Aziz “Stima” na Salum Telela lakini bado wameshindwa kuwa na utulivu mkubwa kwenye eneo hili hasa wanapokwenda kwenda direct play. Hivyo kwenye mchezo wa leo watatakiwa kubadilika kwa maana wanakutana na watu ambao wanajua nini kinatakiwa kufanyika kwenye eneo la kiungo pia ni technical aggressive

Mechi zilizopita tatu za Ndanda FC ndani ya Nangwanda

February 11, 2018 Ndanda FC vs Tanzania Prisons 0 - 0

January 13, 2018 Ndanda FC vs Mbao FC 1 - 1

December 30, 2017 Ndanda FC vs Simba SC0 - 2

Safu ya ushambuliaji nayo imekuwa ikichangia kuiangusha timu hii, tatizo la kujipanga sawasawa kwenye eneo la mwisho linawafanya kushindwa kumalizia kazi nyingi zinafanywa na viungo wao hivyo kupoteza nafasi nyingi za kufunga

Kwa upande wa Yanga sc, wao wapo chini ya kocha George Lwandamina na mara nyingi wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-4-2 huku wakiwa na mabadiliko mengi ya kimbinu na kiufundi, kwa sasa imekuwa sio timu inayochezea sana mpira mara nyingi huenda kwenda direct play huku wakisuma mipira kwenye advanced position ili kufanya attempting ndio wameonekana kuwa hatari sana kwa mpinzani

Safu yao ya ulinzi bado imekuwa na makosa ya kushindwa kujipanga kwa wakati hali inayopelekea wakati fulani kuruhusu magoli mepesi kufungwa, mabàdiliko yà kumrudisha chini Said Juma “Makapu” yameonekana kuinufaisha safi hii akijaribu kuifanya icheze kwa utulivu huku akisaidia sana kufanya Build up kuanzia chini

Eneo la kiungo

Hapa ndipo kwenye roho ya Yanga sc katika patterns zote mbili (Offensive and Defensive) watu kama Papy Kabamba, Raphael Daud na Pius Buswita wamekuwa na muunganiko mzuri sana wa kimbinu kutokea katikati ya kiwanja. Papy Kabamba amekuwa ndiye afisa mipango wa timu kwa sasa, yeye ndiye huamua timu ishambulie kwa wakati gani au ibakie katikati ya kiwanja, hucheza kama kiungo wa ulinzi timu inapopoteza mpira lakini pia hucheza kama kiungo mchezeshaji pale timu inapokuwa na mpira (Box to box midfielder)

Safu ya ushambuliaji

Hii sehemu nyingine inayoibeba timu hii kwa sasa licha ya kumkosa mshambuliaji halisi wa kati, lakini wamekuwa wakijaribu kutumia nafasi kadhaa zinazotengenezwa, leo watamkosa Obrey Chirwa lakini sio tatizo kubwa sana kwao kutokana na kucheza sana kimbinu kwa sasa, Pius Buswita ataendelea kutumika kama false 9 huku Raphael Daud akisimama kama False 10, Ibrahim Ajib akitokea pembeni lakini akicheza kama Auxiliary attacker ama play maker kwenye eneo hili, Emmanuel Martin pia namtazama ni mtu ambaye ataendelea kuwa msaada mkubwa kwenye eneo hili.

Mechi Tatu zilizopita za Yanga

February 14, 2018Young Africans SC vs Majimaji FC 4 - 1 Dar es Salaam

February 6, 2018 Young Africans SC vs Njombe Mji 4 - 0 Dar es Salaam

February 3, 2018 Lipuli FC vs Young Africans SC 0 - 2 Iringa

Yanga wanaweza kufaidika sana katika mchezo huu kutokana uwepo wa watu wengi wenye kasi na uwezo wa kufunga, pia Technical Aggressive hii itawanyima Uhuru Ndanda FC katika kujenganga mashambulizi yao kuanzia chini hivyo kupoteza umiliki wa mpira

Kandanda

Comments

Popular posts from this blog