CHIRWA ATACHEZA AU HATACHEZA DHIDI YA NDANDA? majibu toka yanga haya hapa

Chirwa atacheza au hatacheza dhidi ya Ndanda? Majibu toka Yanga haya hapa
Yanga leo atashuka uwanjani katika uwanja wa Nangwanda Sijaona kumenyana na Ndanda ambao ndiyo wenyeji wa Mchezo huo wa Ligi Kuu VPL 2017/2018.

Kuelekea pambano hilo Klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake wa kamati ya Mashindano Hussein Nyika amesema kuwa Mshambuliaji Obrey Chirwa ataendelea kukosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Ndanda.

Sababu 2 za Chirwa kukosekana leo
Nyika msomaji wa Football Swahili page amesema Chirwa ukiachana na Kuwa majeruhi amabaye anaendelea kurecover bado pia anakosa sifa hata kama angekuwa mzima kwani anakai tatu za Njano zinazomfanya kukosa Sifa ya Kucheza mchezo wa Leo.

” Chirwa atakosekana katika mchezo dhidi ya Ndanda ukiachana na kuwa majeruhi hali iliyomfanya kukosa mchezo wa FA dhidi ya Maji Maji lakini Pia mchezo wa Ndanda hata angekuwa kapona bado anakosa sifa kutokana na kuwa na kadi 3 za Njano “ alimaliza Nyika

Comments

Popular posts from this blog