Posts

Showing posts from October, 2018

MLIPILI AIBUKA NA KUKANA KUTOWEKA SIMBA SC

Image
Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa beki wa aliyefanya vizuri klabuni hapo msimu uliopita, Yusuf Mlipili hajulikani alipo toka October 20 mwaka huu ameibuka na kusema huo ni uzushi yeye yupo Simba na ataendelea kuwepo. Mlipili amesema kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa kwamba alikuwa ameikacha timu na kuelekea 'kusikojulikana'. Mlipili aliyetua Simba Sc misimu miwili iliyopita akitokea Toto Africans ya Jijini Mwanza, hakuonekana kwenye kikosi cha Simba kwa siku kadhaa, na walipoulizwa vingozi wa timu hiyo walisema kuwa hawajui alipo. Hivi karibuni Mlipili alikiri kuwa na wakati mgumu kumshawishi kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameweze kumjumuisha kwenye kikosi cha kwanza. "Nipo na nitaendelea kuwepo ondoeni hofu watu wangu ni uzushi tu mimi kutokuwepo mazoezini. Simba Nguvu moja kila hatua duaaa," amesema Mlipili kupitia ukurasa wake wa Instagram.

KASEJA, MGOSI WAITWA TIMU YA TAIFA

Image
Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Soccer Beach), ambayo imefuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2018), imepangwa kundi B pamoja na bingwa mtetezi Senegal. Akiongea mapema leo October 31, 2018, wakati anataja kikosi kitakachoingia kambini kwaajili ya kujiandaa na fainali hizo, kocha wa timu hiyo Boniface Pawasa amesema wamepangwa kundi gumu lakini haiwakatishi tamaa. ''Tumepangwa kundi gumu sana ambalo lina bingwa mtetezi Senegal pamoja na Nigeria ambaye alicheza fainali na Senegal hivyo sisi tutakuwa timu ndogo kwenye kundi hilo lakini tutajiandaa kwaajili ya kushindana na kuhakikisha tunafanya vizuri'', amesema Pawasa. Michuano hiyo itafanyika nchini Misri kuanzia Desemba 8-14, 2018 katika fukwe za mjini Sharm El Sheikh. Boniface Pawasa ameita wachezaji 18 ambao watajiandaa kufuzu AFCON. Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi hiko ni kipa Juma Kaseja ambaye kwa sasa anacheza Ligi Kuu katika klabu ya KMC. Mwingine ni Muss...

BANKA KUANZA KUITUMIKIA YANGA MWAKANI ADHABU YA KUFUNGIWA IKIISHA

Image
Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ilimfungia kwa miezi 14 kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania baada ya kumkutana hatia ya kutumia mihadarati. Banka aliyetua Yanga msimu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alikutwa na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, aina ya Bangi Desemba 9 mwaka jana baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya. Imejulikana kuwa Mohammed Issa Juma 'Banka' ataruhusiwa kuendelea kucheza soka ifikapo February 8 mwakani ambapo adhabu yake ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi 14 itakuwa imeisha. Katika michuano hiyo, Banka aliisaidia Zanzibar kufika fainali baada ya kufunga bao la ushindi kwa penalti dakika ya 58 Heroes wakiilaza Uganda 2-1 December 15 Uwanja wa Moi mjini Kisumu katika mchezo wa Nusu Fanali. Katika michezo huo Zanzibar walitangulia kwa bao la Makame dakika ya 23 kabla ya Derick Nsibambi kuisawazishia The Cranes dakika ya 29 na n...

YANGA SC 1-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 30/10/2018)

Image

MANENO YA ZAHERA BAADA YA USHINDI DHIDI YA LIPULI

Image
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara hapo jana kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kupata ushindi huo. Zahera amesema licha ya timu yake kuibuka na ushindi mwembamba amefurahishwa na upambanaji unaoendelea kuonyeshwa na wachezaji kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo Amesema kwenye kila mchezo lengo lao la kwanza ni kuibuka na ushindi bila ya kujali idadi ya mabao watakayofunga. Katika hatua nyingine Zahera amewataka waandishi wa habari kulinganisha taarifa zao na sio kuandika kwa lengo la kufanya uchonganishi Zahera amesema waandishi wa habari wamekuwa wakiandika zaidi 'ukosoaji' wake kwa baadhi ya wachezaji bila ya kuandika mazuri yao "Nilisema Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye akili nyingi ya mpira kuliko wachezaji wenu wote hapa Tanzania, lakini sikuona mkiandika hilo" "Mmekuwa mkiandika yale ya kukosoa tu ambayo nayo kimsingi ni ya kumjenga yeye il...

AMBOKILE KIROHO SAFI KUTUA YANGA

Image
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba yule straika wa Mbeya City wanayemfukuzia kwa udi na uvumba, Eliud Ambokile, amekubali kiroho safi kujiunga na kikosi chao. Ambokile, ambaye amekuwa akihusishwa sana kujiunga na Wanajangwani hao, amesema yeye ni mchezaji halali wa Mbeya City na kama Yanga wanamtaka waende wakazungumze na timu yake na yeye atakuwa tayari kuvaa jezi za kijani na njano. Akizungumza na Gazeti la DIMBA Jumatano, Ambokile alisema licha ya kwamba taarifa hizo za kutakiwa na Yanga anazisikia mitaani, lakini hazimzuii yeye kukubali kujiunga na timu hiyo kongwe, kwani ndiyo moja ya malengo yake katika soka. “Niseme wazi kwamba taarifa hizo za kutakiwa na Yanga nazisikia tu kwenye vyombo vya habari, mimi hawajanifuata ili tuzungumze, ninachoweza kusema bado nina mkataba na Mbeya City, lakini kama watazungumza na kumalizana nao sitakuwa na pingamizi”. Yanga wanahusishwa kuifukuzia saini ya straika huyo kutokana na umahiri wake wa kucheka na nyavu ili akaungan...

LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA 12 KUKAMILIKA LEO JUMATANO

Image
Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) inatarajiwa kuendelea leo Jumatano ya October 31 kwa mchezo nmoja tu unaokamilisha raundi ya 12. Baada ya Ligi hiyo kuendelea juzi na jana msimamo wa ligi unaonesha Azam akiendelea kushikilia usukani kwa jumla ya pointi 27 baada ya michezo 11, huku Yanga ikirejea kwenye nafasi yake ya pili ikiwa na ponti 25 baada ya michezo 9 na Simba ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 23 baada ya michezo 10. Mchezo huo unaokamilisha raundi ya 12 mzunguko wa kwanza wa msimu huu wa 2018/2019 utazikutanisha KMC ya Dar es salaam dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 16:09 kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO YA OCTOBER 31-2018

Image
Klabu ya Chelsea inaazimia kumsajili Suso, mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool, mwezi Januari. (Express, kupitia Tutto Mercato Web) Paris St-Germain inapania kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, kutoka Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun) Meneja wa wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambaye pia amewahi kuongoza klabu ya Everton Roberto Martinez anapigiwa upatu kuwa meneja mpya wa kudumu wa Real Madrid. (Mail) Wachezaji wa Tottenham wanahofia huenda meneja wao Mauricio Pochettino, ambaye amehusishwa na klabu za Real Madrid na Manchester United, akaondoka klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Telegraph) Mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi kudai klabu hiyo ya Uturuki inataka mchezaji huyo wa miaka 25 kurejea kwenye klabu hiyo ya Merseyside mwezi Januari. (Liverpool Echo) Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Michael Laudrup amekataa wito wa...

SAMATTA AMFUKUZISHA KARIUS BESIKTAS

Image
Klabu ya Besiktas imeamua kumrejesha kipa huyo, Karius ambaye yupo hapo kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Liverpool na badala yake wakimhitaji Divock Origi. Miamba hiyo ya Uturuki imeripotiwa kuwa imechoshwa na huduma yake na hivyo tayari imefanya mazungumzo na Liverpool kuona namna ya kumrejesha ili kubadilishana na Divock Origi. Karius ambaye ameonekana kutokuwa na matokeo mazuri toka kutua kwake ndani ya klabu ya Besiktas haswa matokeo mabovu ya Europa League dhidi ya KRC Genk ambapo alikubali kipigo cha mabao 4 – 1 huku mshambuliaji hatari wa Tanzania Mbwana Samatta akiweka kimyani mabao mawili atarejea Anfield mwakani mwezi Januari. Mlindalango huyo raia wa Ujerumani yupo kwenye miamba hiyo ya soka ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili ambayo timu hiyo ilipewa nafasi ya kumnunua moja kwa moja baada uwepo wake kwa mkopo ukimalizika. Karius anakumbukwa zaidi baada ya kuizawadia Real Madrid jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali wa Champions League...

NIYONZIMA KIKAANGONI SIMBA SC

Image
Kiungo wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima amewekwa kikaangoni baada ya kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali. Kwa muda mrefu Niyonzima amekuwa kwenye sintofahamu na mabosi wake huku tangu alipojiunga na wenzake mazoezini hajacheza. Mwanaspoti ambalo lilikuwepo eneo la tukio, limeshughudia kiungo wa huyo na nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda, akitoka kuhojiwa na Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Kova. Kova, ambaye amepata kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, aliongoza kikao hicho akiwa na wajumbe wengine wanne kwenye ukumbi wa hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa Niyonzima aliitwa na kamati hiyo kwa ajili ya kuzungumza masuala ya nidhamu yake huku ikielezwa kuwa pande zote zimeshindwa kufikia mwafaka. Chanzo chetu ndani ya kikao hicho kimeeleza kuwa, Kamati ya Kova ilikutana na kigingi baada ya kiungo huyo ku...

JIFUNZE HAPA MAJUKUMU YAKO MME/ MKE UWAPO KWENYE NDOA

Image
Ndoa ni haja ya kawaida kwa kila mwanadamu. Ndoa ndio njia pekee ya kujenga familia, ndoa ndio njia halali ambayo binadamu yeyote anaruhusiwa kutimiza haja zake kimwili tofauti na hapo.... Kwani Mwanaume ameubwa kwa ajili ya mwanamke hali kadhalika mwanamke ameubwa kwa ajili ya mwanaume "Bwana Mungu akasema si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye, Bwana Mungu akamletea Adam usingizi, naye akalala; kisha akatwaa ubavu mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adam Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adam; kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe na watakuwa kitu kimoja (Mwanzo 2:18.....24) Lakini kwa sasa hakuna suala gumu, tata na nyeti linalohusu maisha ya watu kama ndoa. Kumekuwa na migongano mingi na mizozo isiyo kwisha katika maisha ya ndoa. Leo ndoa imeonekana kama utumwa, mzigo au kubebeshwa msalaba, na sasa imekuwa kawaida watu kufunga ndoa saa sita mchana kufika saa 12 jioni ndo...

PAUL NONGA ATAJA SABABU YA KUPOTEZA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA

Image
Mshambuliaji wa Lipuli Fc, Paul Nonga amesema kuwa kilichowafanya washinde kupata ushindi mbele ya Yanga hapo jana ni kushindwa kuzitumia nafasi walizozipata. Nonga amesema kuwa walikuwa wana uwezo wa kufunga ila wamekosea kosa moja ambalo wapinzani wao wametumia nafasi hiyo waliyoipata. "Tumecheza mpira tumejituma, tumeshindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata kutokana na kupoteza umakini hasa kwa nafasi ambazo tumezitumia, tumeona makosa yetu tutafanya vizuri mechi zetu zijazo," alisema. Lipuli wamepoteza mchezo wao mbele ya Yanga baada ya kushinda mchezo wao uliopita dhidi ya Mbao hali iliyowafanya wajiamini zaidi. Katika chati ya msimamo Lipuli wako nafasi ya 13 wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo 11.

FEI TOTO ATAJA SIRI YA USHINDI WAO DHIDI YA LIPULI

Image
Kiungo mkabaji wa klabu  ya Yanga Feisal Salim 'Fei Toto' amesema kuwa ushindi walioupata jana dhidi ya wageni wao Lipuli Fc umetokana na umakini wa wachezaji hasa kwa kufuata maelekezo ya mwalimu. Fei Toto aliyekuwa ndani ya kikosi hicho kilichofanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa. "Namshukuru Mungu tumemaliza mchezo salama, kikubwa ni umakini wa wachezaji hasa katika kufuata maelekezo ya mwalimu hali ambayo imetupa matokeo," alisema Feisal ambaye ametua Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar. Aidha huo ni mchezo wa 9 kwa Yanga na katika michezo hiyo 9 wamefanikiwa kushinda michezo mianane na sare moja.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA OCTOBER 31-2018

Image

HISTORIA YA ALIYEKUWA MMILIKI LEICESTER CITY VICHAI SRIVADDHANAPRABHA

Image
Vichai Srivaddhanaprabha ni Mfanyabiashara na bilionea aliyezaliwa juni 5 mwaka 1958, miaka 60 iliyopita katika jiji la Bangkok nchini Thailand pia ndio C.E.O na Operetor wa kampuni ya King Power International Group ambayo inajishughulisha na maduka ya uuzaji wa vyakula kama SupperMarket na Shoppers. Mnamo mwaka 2015 King Power ilizindua tovuti ya kuagizia vitu bure na nyingine ya kuagizia vitu kwa kulipia,baada ya kuanzishwa mwaka 1989. Mnamo December 2009, kampuni ya King Power ilipokea kibali cha kifalme kutoka kwa mfalme wa Thailand katika sherehe ziliyohudhuria na Raksriaksorn, pia aliwahi kuorodheshwa na jarida la Forbes kuwa tajiri nambari 7 katika taifa hilo la Thailand akiwa na utajiri uliokadiriwa kufikia US dola Bilioni 3.3. Agosti 2010, muungano wa uwekezaji wa soka wa barani Asia akiwa ni pamoja na Srivaddhanaprabha na mwanawe Aiyawatt walikubaliana kununuliwa kwa klabu ya Ligi ya Soka ya nchini Uingereza Leicester City, wakati huo ikicheza ligi ya Championships. ...

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA OCTOBER 30-2018

Image
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara🇹🇿 baada ya kukamilika kwa michezo tisa za raundi ya 12. Kesho utapigwa mchezo mmoja unaokamilisha raundi ya 12.

MAKAMBO AILINDA REKODI YA YANGA TAIFA

Image
Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni wao Lipuli Fc ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Huu unakuwa ni mchezo tisa kwa Yanga, mpaka sasa Yanga imefanikiwa kumeshinda michezo nane na kutoa sare moja, hivo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu. Yanga wamepata bao hilo la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wao Mcongomani Heritier Makambo kwenye dakika ya 10 akipokea pasi kutoka kwa Mrisho Khalfan Ngassa. Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili ambayo ilikuwa imekaliwa na Simba toka jana baada ya kuwapapasa Ruvu Shooting mabao 5-0. Mpaka sasa Yanga wamecheza michez 9 na kujikusanyia pointi 25 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa pointi 23 baada ya michezo 10. Azam Fc ndio vinara wa Ligi hiyo wakikusanya pointi 27 baada ya 11. Mchezo mwingine uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza umeisha kwa sare ya mabao 2-2 kati wa wemyeji Mbao Fc dhidi ...

DKT. MENGI KUANZISHA KIWANDA CHA KUTENGENEZA SMARTPHONE NCHINI

Image
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Dk. Regnald Mengi ametambulisha ujio wa kampuni yake mpya ambayo itakuwa ni ya kwanza Tanzania kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali za Kielektroniki, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi, simu janja (Smartphones), computers, Ipads, music bluetooth speakers, headphones, earphones . Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dk Mengi amesema simu ambazo zitatengenezwa zitakuwa zinakaa na charge kwa zaidi ya wiki moja zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hasa vijijini pia aina hizo za simu zitatumika kama power Bank kucharge simu zingine. Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi mitatu ijayo. Aidha ameeleza kuwa wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 2000 rasmi na zisizo rasmi na kampuni itatoa kipaumbele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye sifa stahiki...

RONALDO AMPIGA CHINI SELENA GONEZ KWA FOLLOWERS INSTAGRAM

Image
Hatimaye muimbaji Selena Gomez ameondolewa usukani wa watu wenye followes wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Mreno Cristiano Ronaldo ambaye anakipiga kunako klabu ya Juventus kwa sasa ndiye anaongoza akiwa na followers Milioni 144 sawa na Selena Gomez ila kuna tofauti. Ronaldo amefikisha followers 144,305,164+huku Selena akiwa na 144,304,857+. Hivyo sasa Cristiano Ronaldo ndiye anakuwa mtu mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram duniani kote. Tazama chini watu wengine 10 wenye followers wengi zaidi kwenye mtandao huo.

NAFASI ZA KAZI ZILIZOTANGAZWA LEO JUMANNE OCTOBER 30-2018

Image
BONYEZA LINKS ZIFUATAZO KUSOMA ZAIDI NA KUAPPLY: Job Opportunity at Project Zawadi, Student Counselor Job Opportunity at Halotel, Product Development And Business Analyst Officer Job Opportunity at Halotel, Digital Payment Expert Job Opportunity at African Underground Mining Services Ltd (AUMS), Mine Software Technician / Trainer Job Opportunity at African Underground Mining Services (AUMS), Long Hole Operator / Trainer Job Opportunity at African Underground Mining Services (AUMS), Shotcrete Sprayer Job Opportunities at African Underground Mining Services (AUMS), Agi Operators Job Opportunity at Swift Momentum, Pre Post Sales Engineer Job Opportunity at Nokia, CS Core Support Engineer Job Opportunity at One Acre Fund, Tanzania Procurement Specialist Job Opportunity at DRG Tanzania, Customer Service Representative Job Opportunity at UNHCR, Field Security Adviser Deputy Managing Director, Operations and Customer Services Job Dar es salaam at CRDB Bank Plc Nafasi zingine ingia  www....

SERENGETI BOYS YAANZA KUUSAKA UBINGWA COSAFA

Image
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' ipo katika maandalizi ya kuelekea mashindano ya vijana ya mataifa yaliyo kusini mwa Afrika 'COSAFA' mwezi Disemba. Mashindano hayo yatafanyika nchini Botswana ambapo Serengeti Boys inatarajia kushiriki kama mwalikwa. Yatakuwa ni mashindano ya kwanza ya nje ya Afrika Mashariki kwa timu hiyo kushiriki baada ya kumalizika kwa michuano ya CECAFA U-17 Challenge ambayo Serengeti Boys iliondolewa katika hatua ya nusu fainali. Akizungumza kuelekea michuano hiyo, kocha mkuu wa timu hiyo Oscar Milambo amesema, "Timu hii toka tumeanza kuijenga hatujawahi kucheza michezo ya kirafiki au ya kimashindano tofauti na ukanda wetu wa Afrika Mashariki na kati, kwahiyo kwa kwenda kucheza kwenye nchi za kusini mwa Afrika tunategemea kwamba tutakutana na changamoto mpya kitu ambacho kitatupa dira ya kuona kwenye maandalizi tumefikia kiwango gani". "Limekuwa ni jambo la faraja kwamba tumepata nafasi ya kwenda k...

RONALDO ATAJA SABABU YA YEYE KUHAMIA JUVENTUS "SI PESA"

Image
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo amesema kuwa aliihama Real Madrid na kujiunga na miamba hiyo ya Italia kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Hispania, Florentino Perez hakumfanya ajihisi kuwa mchezaji anayethaminiwa Santiago Bernabeu. Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, amesema kuwa Perez alikuwa akimtazama kwenye mahusiano ya kibiashara zaidi na hicho ndicho anachotambua hivyo kila alichomuambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake. ”Perez alikuwa akinitazama mimi kwenye mahusiano ya kibiashara zaidi  na hicho ndicho ninachofahamu hivyo kila alichokuwa akiniambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake,” amesema Ronaldo. Raia huyo wa Ureno ameongeza “Nilisikia ndani ya klabu, hasa kutoka kwa rais mwenyewe kwamba hawakunichukulia mimi sawa na vile walivyofanya wakati nakuja kwenye miaka minne au mitano iliyopita.” “Rais alikuwa akinitazama, macho yake yakitoa tafsri ambayo haiyendani na kile anachozungumza, kiasi kwamba sikuwa na nafasi tena kwao. Kama unaelewa ninachomaanisha, hich...

KIKOSI CHA LIPULI FC DHIDI YA YANGA

Image
Kikosi cha Lipuli Fc dhidi ya Yanga leo saa 19:00 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. 1:Mohamed Yusuph 2:William Lucian 3:Paul Ngalema 4:Ibrahim Job 5:Joseph Owino 6:Novaty Lufunga 7:Miraji Athuman 8:Jimishoji Mwasondola 9:Paul Nonga 10:Issa Rashid 11:Zawadi Mauya Kikosi cha Akiba 1:Abdallah Makangana 2:Steve Mganga 3:Mussa Nampaka 4:Seif Abdallah Karie 5:Daluwesh Saliboko 6Yusuph Wehed 7:Shaban Adda Samweli Moja- Kocha Mkuu Seleman Matola- Kocha Msaidizi

NIYONZIMA AWASHANGAA WAANDISHI WA HABARI

Image
Baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Kamati ya nidhamu ya klabu ya Simba inayoongozwa na Suleimani Kova imemwita na kumhoji kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Haruna Niyonzima kufuatia uwepo wa madai ya utovu wa nidhamu, Niyonzima amefunguka kuhusu tuhuma hizo. Habari hizo ziliendelea kueleza kuwa Niyonzima aliitwa na kuhojiwa huku ikielezwa pande zote zimeshindwa kufikia muafaka, kamati ilikutana na kigingi baada ya kiungo huyo kuonyesha mkataba wake ambao anadai mabosi wake wameshindwa kuutimiza matakwa ya mkataba kama walivyokubaliana. HARUNA NIYONZIMA AMESEMA👇👇👇 “Mimi ata sijui ila sijaongea nao unajua waandishi wa hapa wana matatizo sana,ila nitadili nao waache” “nipo salama na klabu yangu na kutopangwa ni jambo la kawaida na sipo peke yangu . Muda utafika nitacheza . Hayo ya kusema nimekaa kikao na klabu kuhusu mimi kugoma siyajui kabisa “

HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA LIPULI FC

Image
Kikosi cha Yanga dhidi ya Lipuli Fc leo saa 19:00 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. 1:Beno Kakolanya 2:Paul Godfrey 3:Gadiel Michael 4:Abdallah Shaibu 'Ninja' 5:Kelvin Yondani (C) 6:Feisal Salum 'Fei Toto' 7:Mrisho Ngassa 'Anko' 8:Maka Edward 9:Heritier Makambo 10:Thabani Kamusoko 11:Matheo Antony Kikosi cha Akiba 1:Klaus Kindoki 2:Juma Abdul 3:Raphael Daud 4:Said Juma Makapu 5:Amissi Tambwe 6:Deus Kaseke 7:Jafary Mohammed

KESI INAYOWAKABILI VIONGOZI WATATU WA SIMBA KUANZA KUSIKILIZWA

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesho Jumatano ya October 31 itaanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya kughushi na kutakatisha fedha inayowakabili viongozi watatu wa Klabu wa Simba. Washtakiwa hao ni Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva, makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe. Hatua hiyo inatokana na upande wa mashtaka kumaliza kuwasomea maelezo ya awali (PH) na hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, kupanga October 31, 2018 kuanza kisikiliza ushahidi. Kesi hiyo inatokana na matumizi ya pesa za uhamisho wa mchezaji wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi, kwenda Klabu ya Etoile Sportive Du Dahel ya Tunisia, kwa madai ya kutumia pesa hizo kununulia nyasi bandia na gharama za ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo ulioko Bunju. Katika kesi hiyo Hans Poppe anakabiliwa na mashtaka mawili, kughushi nyaraka na kuwasilisha nyaraka za uongo yeye pamoja na wenzake. Wakati, Avena na Nyange wanakabiliw...

KESI YA JAMAL MALINZI NA WENZAKE WANNE KUENDELEA NA USHAHIDI

Image
Kesi ya kula njama, kughushi na kutakatisha fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na wenzake wanne, inatarajia kuendelea na ushahidi. Kesi hiyo jinai namba 213/ 2017 inatarajia kuendelea kesho Jumatano October 31,  2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mbali na Malinzi(57), washtakiwa wengine  ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga (27). Wengine, Meneja wa  Ofisi za TFF, Miriam  Zayumba na Karani wa TFF,  Flora Rauya ambao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000. Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wa...

TFF KUSAFIRISHA WANDISHI WA HABARI 15 KWA BASI KWENDA LESOTHO

Image
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa nafasi 15 za usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari kwenda Lesotho kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Kwenye mchezo huo wa kundi L katika kuwania kufuzu AFCON 2019 utakaochezwa November 18 mwaka huu Tanzania watakuwa wageni wa Lesotho. Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kwamba shirikisho hilo litatoa usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari za Michezo kwenda na kurudi Lesotho, lakini watajigharamia kula na malazi. “Gharama nyingine zote za Visa, malazi, Chakula na nyingine zisizohusu usafiri itakuwa gharama ya msafiri mwenyewe (Mwandishi au Chombo).  Nafasi zipo 15 na safari itaanza November 13,2018, kwa anayetaka kwenda afanye mawasiliano kupitia na Idara ya Habari ya TFF,” amesema Ndimbo. TFF pamoja na kutaka mashabiki wasafiri kwa wingi kwenda kuisapoti timu, lakini inawasaidia na Waandishi wa Habari waweze kwenda kuripoti mchezo huo muhimu unaoweza kuwa wa kihistoria endapo ...

UCHAGUZI MKUU SIMBA WABADILISHA RATIBA

Image
Kuelekea Uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba unaoatarajia kufanyika November 4 mwaka huu, uongozi wa klabu hiyo umeomba mabadiliko ya mechi yao dhidi ya JKT Tanzania iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi huo. Awali, Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilitangaza uchaguzi huo kufanyika November 3 lakini baada ya kuangalia ratiba ya Ligi Kuu Bara walibaini tarehe hiyo kutakuwa na mechi hivyo kuamua uchaguzi huo ufanyike November 4. Baada ya mabadiliko hayo ambayo Simba walidhani mechi hiyo ingechezwa uwanja wa Taifa lakini baadaye uongozi wa JKT Tanzania ambao ni wenyeji wa mechi hiyo waliomba mechi yao ichezwe uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Hata hivyo imeoneka kuwepo na ugumu kwa klabu ya Simba kwani mechi hiyo itachezwa Jumamosi ambapo viongozi na wanachama wa klabu hiyo watakuwa Tanga na watalazimika kurejea jijini Dar es Salaam Jumapili kwa ajili ya mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika siku hiyo hiyo ya uchaguzi kuanzia asubuhi na baadaye kupiga kura. Ba...