MAKAMBO AILINDA REKODI YA YANGA TAIFA
Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni wao Lipuli Fc ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Huu unakuwa ni mchezo tisa kwa Yanga, mpaka sasa Yanga imefanikiwa kumeshinda michezo nane na kutoa sare moja, hivo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu.
Yanga wamepata bao hilo la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wao Mcongomani Heritier Makambo kwenye dakika ya 10 akipokea pasi kutoka kwa Mrisho Khalfan Ngassa.
Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili ambayo ilikuwa imekaliwa na Simba toka jana baada ya kuwapapasa Ruvu Shooting mabao 5-0.
Mpaka sasa Yanga wamecheza michez 9 na kujikusanyia pointi 25 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa pointi 23 baada ya michezo 10.
Azam Fc ndio vinara wa Ligi hiyo wakikusanya pointi 27 baada ya 11.
Mchezo mwingine uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza umeisha kwa sare ya mabao 2-2 kati wa wemyeji Mbao Fc dhidi ya Mbeya City.
Mabao ya wenyeji wanapenda kujiita wabishi wa Mwanza yote yamefungwa na Everigestus Mjwahuki dakija ya 83 na dakika ya 4 kati ya zilizoongezwa baada ya dakika 90 kuisha, huku ya Mbeya City yakifungwa Idd Seleman dakika ya 11 na Eliud Ambokile dakika ya 48.

Comments
Post a Comment