SAMATTA AMFUKUZISHA KARIUS BESIKTAS

Klabu ya Besiktas imeamua kumrejesha kipa huyo, Karius ambaye yupo hapo kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Liverpool na badala yake wakimhitaji Divock Origi.

Miamba hiyo ya Uturuki imeripotiwa kuwa imechoshwa na huduma yake na hivyo tayari imefanya mazungumzo na Liverpool kuona namna ya kumrejesha ili kubadilishana na Divock Origi.

Karius ambaye ameonekana kutokuwa na matokeo mazuri toka kutua kwake ndani ya klabu ya Besiktas haswa matokeo mabovu ya Europa League dhidi ya KRC Genk ambapo alikubali kipigo cha mabao 4 – 1 huku mshambuliaji hatari wa Tanzania Mbwana Samatta akiweka kimyani mabao mawili atarejea Anfield mwakani mwezi Januari.

Mlindalango huyo raia wa Ujerumani yupo kwenye miamba hiyo ya soka ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili ambayo timu hiyo ilipewa nafasi ya kumnunua moja kwa moja baada uwepo wake kwa mkopo ukimalizika.

Karius anakumbukwa zaidi baada ya kuizawadia Real Madrid jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali wa Champions League ambapo mashabiki wengi wa majogoo hao wa England wakimtupia lawama kwa kukubali kufungwa mabao mepesi.

Comments

Popular posts from this blog