MANENO YA ZAHERA BAADA YA USHINDI DHIDI YA LIPULI

Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara hapo jana kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kupata ushindi huo.

Zahera amesema licha ya timu yake kuibuka na ushindi mwembamba amefurahishwa na upambanaji unaoendelea kuonyeshwa na wachezaji kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo

Amesema kwenye kila mchezo lengo lao la kwanza ni kuibuka na ushindi bila ya kujali idadi ya mabao watakayofunga.

Katika hatua nyingine Zahera amewataka waandishi wa habari kulinganisha taarifa zao na sio kuandika kwa lengo la kufanya uchonganishi

Zahera amesema waandishi wa habari wamekuwa wakiandika zaidi 'ukosoaji' wake kwa baadhi ya wachezaji bila ya kuandika mazuri yao

"Nilisema Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye akili nyingi ya mpira kuliko wachezaji wenu wote hapa Tanzania, lakini sikuona mkiandika hilo"

"Mmekuwa mkiandika yale ya kukosoa tu ambayo nayo kimsingi ni ya kumjenga yeye ili awe mchezaji mkubwa," alisema Zahera.

Comments

Popular posts from this blog