KASEJA, MGOSI WAITWA TIMU YA TAIFA

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Soccer Beach), ambayo imefuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2018), imepangwa kundi B pamoja na bingwa mtetezi Senegal.

Akiongea mapema leo October 31, 2018, wakati anataja kikosi kitakachoingia kambini kwaajili ya kujiandaa na fainali hizo, kocha wa timu hiyo Boniface Pawasa amesema wamepangwa kundi gumu lakini haiwakatishi tamaa.

''Tumepangwa kundi gumu sana ambalo lina bingwa mtetezi Senegal pamoja na Nigeria ambaye alicheza fainali na Senegal hivyo sisi tutakuwa timu ndogo kwenye kundi hilo lakini tutajiandaa kwaajili ya kushindana na kuhakikisha tunafanya vizuri'', amesema Pawasa.

Michuano hiyo itafanyika nchini Misri kuanzia Desemba 8-14, 2018 katika fukwe za mjini Sharm El Sheikh.

Boniface Pawasa ameita wachezaji 18 ambao watajiandaa kufuzu AFCON.

Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi hiko ni kipa Juma Kaseja ambaye kwa sasa anacheza Ligi Kuu katika klabu ya KMC.

Mwingine ni Mussa Hassan Mgosi ambaye ni kocha wa timu ya vijana ya Simba na wengine ni  Ibrahim Abdallah, Ahmed Juma.

Pawasa alisema kikosi hiko kitaanza mazoezi Jumamosi katika viwanja  vya fukwe ya Coco Beach.

"Nafahamu kuna kuna wachezaji ambao wapo katika majukumu ya klabu zao lakini linapofika suala la Utaifa ni muhimu kuliweka mbele na kama udhuru tutatoa katika wiki moja ya mwanzo kabla timu kuingia kambini na baada ya hapo hatutataka kuona mchezaji anakosekana," alisema Pawasa.

Kikosi hicho kitakuwa na benchi la ufundi ambalo litaongozwa na Pawasa msaidizi wake Adam Katwila, Deo Lucas atakuwa Meneja na Frank Mutago mtunza vifaa.

Wachezaji walioitwa ni:
1:Ibrahim Abdallah
2:Ahmed Juma
3:Juma Ibrahim
4:Roland Msonjo
 5:Samwel Salonge
6:Yahya Tumbo
7:Jarubu Juma
8:Ahmada Ahmada
9:Sudi Ame Sudi
10:Alphat Ndise
11:Kashiru Salum
12:Musa Hassan Mgosi
13:Ally Humud
14:Mohamed Makame
15:Shaffih Mussa
16:Justine Antony
17:Seif Mwinyi
18:Juma Kaseja Juma

Comments

Popular posts from this blog