TFF KUSAFIRISHA WANDISHI WA HABARI 15 KWA BASI KWENDA LESOTHO
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa nafasi 15 za usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari kwenda Lesotho kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kwenye mchezo huo wa kundi L katika kuwania kufuzu AFCON 2019 utakaochezwa November 18 mwaka huu Tanzania watakuwa wageni wa Lesotho.
Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kwamba shirikisho hilo litatoa usafiri wa basi kwa Waandishi wa Habari za Michezo kwenda na kurudi Lesotho, lakini watajigharamia kula na malazi.
“Gharama nyingine zote za Visa, malazi, Chakula na nyingine zisizohusu usafiri itakuwa gharama ya msafiri mwenyewe (Mwandishi au Chombo).
Nafasi zipo 15 na safari itaanza November 13,2018, kwa anayetaka kwenda afanye mawasiliano kupitia na Idara ya Habari ya TFF,” amesema Ndimbo.
TFF pamoja na kutaka mashabiki wasafiri kwa wingi kwenda kuisapoti timu, lakini inawasaidia na Waandishi wa Habari waweze kwenda kuripoti mchezo huo muhimu unaoweza kuwa wa kihistoria endapo Taifa Stars itapata ushindi.
Katika msimamo wa kundi hilo Tanzania ni ya pili ikiwa na pointi 5 nyuma ya kinara Uganda mwenye pointi 10, hiyo ni baada ya kucheza michezo minne ikishinda mmoja, kutoa sare miwili na kupoteza mmoja.

Comments
Post a Comment