KESI YA JAMAL MALINZI NA WENZAKE WANNE KUENDELEA NA USHAHIDI

Kesi ya kula njama, kughushi na kutakatisha fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na wenzake wanne, inatarajia kuendelea na ushahidi.

Kesi hiyo jinai namba 213/ 2017 inatarajia kuendelea kesho Jumatano October 31,  2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Malinzi(57), washtakiwa wengine  ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga (27).

Wengine, Meneja wa  Ofisi za TFF, Miriam  Zayumba na Karani wa TFF,  Flora Rauya ambao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.

Tayari mashahidi nane upande wa mashtaka wametoa ushahidi  wao dhidi ya washtakiwa hao.

Comments

Popular posts from this blog