DKT. MENGI KUANZISHA KIWANDA CHA KUTENGENEZA SMARTPHONE NCHINI
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Dk. Regnald Mengi ametambulisha ujio wa kampuni yake mpya ambayo itakuwa ni ya kwanza Tanzania kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali za Kielektroniki, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi, simu janja (Smartphones), computers, Ipads, music bluetooth speakers, headphones, earphones .
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dk Mengi amesema simu ambazo zitatengenezwa zitakuwa zinakaa na charge kwa zaidi ya wiki moja zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hasa vijijini pia aina hizo za simu zitatumika kama power Bank kucharge simu zingine.
Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi mitatu ijayo.
Aidha ameeleza kuwa wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 2000 rasmi na zisizo rasmi na kampuni itatoa kipaumbele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye sifa stahiki.
Comments
Post a Comment