PAUL NONGA ATAJA SABABU YA KUPOTEZA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA

Mshambuliaji wa Lipuli Fc, Paul Nonga amesema kuwa kilichowafanya washinde kupata ushindi mbele ya Yanga hapo jana ni kushindwa kuzitumia nafasi walizozipata.

Nonga amesema kuwa walikuwa wana uwezo wa kufunga ila wamekosea kosa moja ambalo wapinzani wao wametumia nafasi hiyo waliyoipata.

"Tumecheza mpira tumejituma, tumeshindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata kutokana na kupoteza umakini hasa kwa nafasi ambazo tumezitumia, tumeona makosa yetu tutafanya vizuri mechi zetu zijazo," alisema.

Lipuli wamepoteza mchezo wao mbele ya Yanga baada ya kushinda mchezo wao uliopita dhidi ya Mbao hali iliyowafanya wajiamini zaidi.

Katika chati ya msimamo Lipuli wako nafasi ya 13 wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo 11.

Comments

Popular posts from this blog