TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO YA OCTOBER 31-2018
Klabu ya Chelsea inaazimia kumsajili Suso, mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool, mwezi Januari. (Express, kupitia Tutto Mercato Web)
Paris St-Germain inapania kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, kutoka Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)
Meneja wa wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambaye pia amewahi kuongoza klabu ya Everton Roberto Martinez anapigiwa upatu kuwa meneja mpya wa kudumu wa Real Madrid. (Mail)
Wachezaji wa Tottenham wanahofia huenda meneja wao Mauricio Pochettino, ambaye amehusishwa na klabu za Real Madrid na Manchester United, akaondoka klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Telegraph)
Mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi kudai klabu hiyo ya Uturuki inataka mchezaji huyo wa miaka 25 kurejea kwenye klabu hiyo ya Merseyside mwezi Januari. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Michael Laudrup amekataa wito wa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Uhispania. (AS)
Winga wa Wales Gareth Bale, 29, ameongoza kura ya mashabiki wa Real Madrid kuhusu mchezaji aliyefanya vibaya zaidi msimu huu. (Marca)
Mshambuliaji wa Reiss Nelson, 18, ambaye yuko Hoffenheim kwa mkopo amepuuza madai kwamba huenda akaondoka klabu hiyo na kuhamia ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani. (Independent)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anatarajia klabu hiyo imnunulie mlinzi wa kati mwezi Januari wakati dirisha la uhamisho wa washezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)
Juventus ina mpango wa kumsajili mchezaji wa Colombia James Rodriguez mwezi Januari mwakani ikiwa Bayern Munich itaridhia kukatiza makubaliano ya kiungo huyo wa miaka 27 kutoka Real Madrid kwa mkopo. (Mail)
Kuna tetesi kuwa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 29, "alikosa kuhudhuria mkutano wa pamoja wa wachezaji au kukataa kushiriki mazoezi ya mwisho" kushinikiza uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund hadi Gunners.
Hayo ni kwa mujibu wa meneja wa zamani wa klabu hiyo ya Ujerumani, Peter Stoger. (Mirror, via Bulinews)
Neymar, 26, amesema meneja wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel alikuwa sawa kuwaacha nje ya kikosi mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, na Adrien Rabiot, 23, wakati wa mechi dhidi ya Marseille baada ya wachezaji hao kuchelewa kufika kwa mkutano wa timu. (Mail)
Manchester United ahaitamuajiri mkurugenzi kandanda hadi pale meneja Jose Mourinho atakapoidhinisha hatua hiyo. (ESPN)
Paul Mitchell ambaye ni Mkuu wa usajili na maendeleo katika klabu ya RB Leipzig, amesema hajawasiliana Manchester United kuhusu uwezekano yeye kupewa wadhifa wa mkurugenzi wa soka katika uga wa Old Trafford. (Manchester Evening News)
Mitchell pia anasema RB Leipzig inapania kumsajili mshambuliaji wa Everton forward Ademola Lookman, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopomsimu uliyopita. Hilo litafanyika endapo kiungo huyo wa miaka 21 ataamua kuondoka Goodison Park. (Sun)

Comments
Post a Comment