FEI TOTO ATAJA SIRI YA USHINDI WAO DHIDI YA LIPULI

Kiungo mkabaji wa klabu  ya Yanga Feisal Salim 'Fei Toto' amesema kuwa ushindi walioupata jana dhidi ya wageni wao Lipuli Fc umetokana na umakini wa wachezaji hasa kwa kufuata maelekezo ya mwalimu.

Fei Toto aliyekuwa ndani ya kikosi hicho kilichofanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa.

"Namshukuru Mungu tumemaliza mchezo salama, kikubwa ni umakini wa wachezaji hasa katika kufuata maelekezo ya mwalimu hali ambayo imetupa matokeo," alisema Feisal ambaye ametua Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar.

Aidha huo ni mchezo wa 9 kwa Yanga na katika michezo hiyo 9 wamefanikiwa kushinda michezo mianane na sare moja.

Comments

Popular posts from this blog