BANKA KUANZA KUITUMIKIA YANGA MWAKANI ADHABU YA KUFUNGIWA IKIISHA

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ilimfungia kwa miezi 14 kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania baada ya kumkutana hatia ya kutumia mihadarati.

Banka aliyetua Yanga msimu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alikutwa na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, aina ya Bangi Desemba 9 mwaka jana baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya.

Imejulikana kuwa Mohammed Issa Juma 'Banka' ataruhusiwa kuendelea kucheza soka ifikapo February 8 mwakani ambapo adhabu yake ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi 14 itakuwa imeisha.

Katika michuano hiyo, Banka aliisaidia Zanzibar kufika fainali baada ya kufunga bao la ushindi kwa penalti dakika ya 58 Heroes wakiilaza Uganda 2-1 December 15 Uwanja wa Moi mjini Kisumu katika mchezo wa Nusu Fanali.

Katika michezo huo Zanzibar walitangulia kwa bao la Makame dakika ya 23 kabla ya Derick Nsibambi kuisawazishia The Cranes dakika ya 29 na ndipo ‘Mo Banka’ akawazima Waganda kipindi cha pili.

Na kwenye fainali, pamoja na kucheza vizuri, Zanzibar wafungwa na wenyeji, Kenya kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Kenyatta huko Machakos.

Comments

Popular posts from this blog