UCHAGUZI MKUU SIMBA WABADILISHA RATIBA
Kuelekea Uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba unaoatarajia kufanyika November 4 mwaka huu, uongozi wa klabu hiyo umeomba mabadiliko ya mechi yao dhidi ya JKT Tanzania iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi huo.
Awali, Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilitangaza uchaguzi huo kufanyika November 3 lakini baada ya kuangalia ratiba ya Ligi Kuu Bara walibaini tarehe hiyo kutakuwa na mechi hivyo kuamua uchaguzi huo ufanyike November 4.
Baada ya mabadiliko hayo ambayo Simba walidhani mechi hiyo ingechezwa uwanja wa Taifa lakini baadaye uongozi wa JKT Tanzania ambao ni wenyeji wa mechi hiyo waliomba mechi yao ichezwe uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Hata hivyo imeoneka kuwepo na ugumu kwa klabu ya Simba kwani mechi hiyo itachezwa Jumamosi ambapo viongozi na wanachama wa klabu hiyo watakuwa Tanga na watalazimika kurejea jijini Dar es Salaam Jumapili kwa ajili ya mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika siku hiyo hiyo ya uchaguzi kuanzia asubuhi na baadaye kupiga kura.
Baada ya kulitazama hilo, uongozi wa Simba umeamua kuiandika barua Bodi ya Ligi ambao ndiyo wasimamizi wa ligi hiyo kuomba mechi yao irudishwe nyuma na kuchezwa Ijumaa ya October 2.
Baada ya kuandika na kuituma barua hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Boniface Wambura amekiri kupokea barua hiyo na kwamba wanaifanyia kazi.
"Tumepokea barua ya Simba leo (jana) Jumatatu asubuhi, bado hatujaifanyia kazi ila tutaifanyia kazi na kuwajibu," alisema Wambura.
Kaimu Rais w aSimba, Salim Abdallah alisema wamelazimika kuomba mechi hiyo ichezwe Ijumaa kwani ratiba yao imewabana.
"Haitakuwa rahisi tucheze Jumamosi halafu tuwahi kwenye Mkutano mkuu na uchaguzi siku ya Jumapili, kwanza kuna mambo tutakuwa hatujaweka sawa, hivyo tumewaomba na tunasubiri majibu yao," alisema Try Again
Naye Afisa Habari wa JKT Tanzania, Koplo Jamila Mutabazi alisema bado hawajapokea taarifa wala maombi yoyote kutoka Simba juu ya mechi hiyo na endapo watapata basi watajadili na viongozi na kutolea maamuzi.

Comments
Post a Comment