MLIPILI AIBUKA NA KUKANA KUTOWEKA SIMBA SC

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa beki wa aliyefanya vizuri klabuni hapo msimu uliopita, Yusuf Mlipili hajulikani alipo toka October 20 mwaka huu ameibuka na kusema huo ni uzushi yeye yupo Simba na ataendelea kuwepo.

Mlipili amesema kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa kwamba alikuwa ameikacha timu na kuelekea 'kusikojulikana'.

Mlipili aliyetua Simba Sc misimu miwili iliyopita akitokea Toto Africans ya Jijini Mwanza, hakuonekana kwenye kikosi cha Simba kwa siku kadhaa, na walipoulizwa vingozi wa timu hiyo walisema kuwa hawajui alipo.

Hivi karibuni Mlipili alikiri kuwa na wakati mgumu kumshawishi kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameweze kumjumuisha kwenye kikosi cha kwanza.

"Nipo na nitaendelea kuwepo ondoeni hofu watu wangu ni uzushi tu mimi kutokuwepo mazoezini. Simba Nguvu moja kila hatua duaaa," amesema Mlipili kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Comments

Popular posts from this blog